Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 23, 2025


 

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 23, 2025

DOMINIKA YA 7 YA MWAKA C


MWANZO:

Zab. 13:5 – 6

Nami nimezitumainia fadhili zako; moyo wangu na uufurahie wokovu wako. Naam, nimwimbie Bwana, kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.


SOMO 1

1Sam. 26:2,7-9,12-13,22-23

Sauli aliondoka, akashuka nyika kwa Zifu, naye alikuwa na watu elfu tatu, wateule wa Israeli, pamoja naye, ili kumtafuta Daudi katika nyika ya Zefu. Basi Daudi na Abishai wakawaendea watu usiku; na tazama, Sauli alikuwapo kati ya magari amelala usingizi, na fumo lake limechomekwa chini, karibu na kichwa chake; naye Abneri na watu wake wamelala wakimzunguka. Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hata nchi kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili. Lakni Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihi wa Bwana, naye akawa hana hatia? Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia. Kisha Daudi akaenda ng’ambo ya pili, akasimama juu ya kilima, mbali sana; palipokuwapo nafasi tele katikati yao. Daudi akapiga kelele akasema, Litazame fumo hili, Ee mfalme! Kijana mmoja na avukie huku, alitwae. Naye Bwana atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana Bwana amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa Bwana.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI

Zab. 102:1 – 4, 8, 10, 12 – 13 (K) 8


(K) Bwana amejaa huruma na neema.


Ee nafsi yangu umhimidi Bwana.

Naam, vyote vilivyomo ndani yangu

Vilihimidi jina lake takatifu.

Ee nafsi yangu umhimidi Bwana,

Wala usizisahau fadhili zake zote. (K)


Akusamehe maovu yako yote,

Akuponya magonjwa yako yote,

Aukomboa uhai wako na kaburi,

Akutia taji ya fadhili na rehema. (K)


Bwana amejaa huruma na neema,

Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

Hukutenda sawasawa na hatia zetu,

Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. (K)


Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,

Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao. (K)


SOMO 2

1Kor. 15:45 – 49

Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule war oho, bali ule wa asili; baadaye huja ule war oho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Kama alivyoa yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


SHANGILIO

Yn. 13:34

Aleluya, aleluya,

Nawapa amri mpya, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Aleluya.


INJILI

Lk. 6:27-38

Siku ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi hivyo. Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile. Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.

Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; achilieni nanyi mtaachiliwa. Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

3 comments: