MASOMO YA MISA, FEBRUARI 23, 2025
DOMINIKA
YA 7 YA MWAKA C
MWANZO:
Zab.
13:5 – 6
Nami
nimezitumainia fadhili zako; moyo wangu na uufurahie wokovu wako. Naam,
nimwimbie Bwana, kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.
SOMO
1
1Sam.
26:2,7-9,12-13,22-23
Sauli
aliondoka, akashuka nyika kwa Zifu, naye alikuwa na watu elfu tatu, wateule wa
Israeli, pamoja naye, ili kumtafuta Daudi katika nyika ya Zefu. Basi Daudi na
Abishai wakawaendea watu usiku; na tazama, Sauli alikuwapo kati ya magari
amelala usingizi, na fumo lake limechomekwa chini, karibu na kichwa chake; naye
Abneri na watu wake wamelala wakimzunguka. Ndipo Abishai akamwambia Daudi,
Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo
hata nchi kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili. Lakni Daudi akamwambia
Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya
masihi wa Bwana, naye akawa hana hatia? Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile
gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona
jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa
usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia. Kisha Daudi akaenda ng’ambo ya
pili, akasimama juu ya kilima, mbali sana; palipokuwapo nafasi tele katikati
yao. Daudi akapiga kelele akasema, Litazame fumo hili, Ee mfalme! Kijana mmoja
na avukie huku, alitwae. Naye Bwana atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu
wake; maana Bwana amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono
wangu juu ya masihi wa Bwana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
102:1 – 4, 8, 10, 12 – 13 (K) 8
(K)
Bwana amejaa huruma na neema.
Ee
nafsi yangu umhimidi Bwana.
Naam,
vyote vilivyomo ndani yangu
Vilihimidi
jina lake takatifu.
Ee
nafsi yangu umhimidi Bwana,
Wala
usizisahau fadhili zake zote. (K)
Akusamehe
maovu yako yote,
Akuponya
magonjwa yako yote,
Aukomboa
uhai wako na kaburi,
Akutia
taji ya fadhili na rehema. (K)
Bwana
amejaa huruma na neema,
Haoni
hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Hukutenda
sawasawa na hatia zetu,
Wala
hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. (K)
Kama
mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo
alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
Kama
vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo
Bwana anavyowahurumia wamchao. (K)
SOMO
2
1Kor.
15:45 – 49
Ndivyo
ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni
roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule war oho, bali ule wa asili; baadaye
huja ule war oho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili
atoka mbinguni. Kama alivyoa yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na
kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama
tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye
aliye wa mbinguni.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn.
13:34
Aleluya,
aleluya,
Nawapa
amri mpya, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo
hivyo.
Aleluya.
INJILI
Lk.
6:27-38
Siku
ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui
zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao
wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja,
mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila
akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Na kama
mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. Maana mkiwapenda wale
wawapendao ninyi hivyo. Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha
fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. Nanyi
mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye
dhambi hufanya vivyo hivyo. Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu
kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili
warudishiwe vile vile. Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha
msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa
Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
Basi,
iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi
hamtahukumiwa; achilieni nanyi mtaachiliwa. Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa;
kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu
watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho
mtakachopimiwa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
Sifa kwako ee kristo
ReplyDeleteMungu ni mwema
ReplyDeleteLove your enemies
ReplyDelete