“ASALI ITOKAYO
MWAMBANI”
Jumatano , Januari 5,
2022,
Juma kabla ya Epifania
1Yon. 4:11-18
Mk. 6:45-52
KUWA WATU WASIO NA
HILA!
Karibuni sana wapendwa
wa Bwana kwa tafakari ya neno la Bwana asubuhi ya leo. Neno la Bwana katika
somo la injili, tunapata kutafakari habari za wanafunzi wa Yesu wakiwa katika
hofu kubwa, upepo unawasumbua, unawatesa, wanatumia nguvu zao wakipambana nao
bila mafanikio.
Baadaye Yesu
anajitokeza katikati yao na wanapomuona wanaongezeka tena katika hofu badala ya
kupata matumaini. Wanapiga yowe tena wakifikiri kwamba Yesu ni mzima au pepo
mchafu amewavamia. Hofu na wasiwasi waliokuwa nao umewafanya washindwe
kumtambua Yesu wakati wa matatizo yao na kumfananisha na mzimu. Ndivyo
inavyotokea na kwetu kila siku. Wengi wetu tuna hofu na wasiwasi, hivi ni vitu
vibaya sana. Vimetufanya tukose iman na kufanya maamuzi ya ajabu.
Wanafunzi walipokuwa
katika hofu wamefanya maamuzi ya ajabu. Sisi tuogope kufanya maamuzi hasa
wakati tunapokuwa na hofu na wasiwasi mkubwa. Yafaa kwenda mbele ya Mungu kila
ujisikiapo hofu kwani maamuzi yoyote utakayofanya katika hofu na wasiwasi ni
maamuzi yaliyokosa imani. Unapokuwa katika hofu, habari inayozunguka kichwani
yaweza kuwa ni kuhusu pepo wabaya na watu wenye roho mbaya wakitaka kukudhuru.
Kila kitakachotokea utakiona kwa macho ya pekee. Ukiona mjusi chumbani utamwita
pepo mchafu, muda wote utatembea katika wasiwasi. Hata chumbani utashindwa
kulala peke yako. Tujifunze kupambana na hofu zetu.
Katika somo la kwanza,
Yohane anasisitiza kwamba kupendana, na anaeleza kwamba katika pendo hakuna
hofu, hakuna kumdhania mwenzako vibaya. Somo hili linatuhimize juu ya hatari ya
hofu. Tukitaka kuishi na wenzatu katika pendo, tuepuke kumdhania vibaya na hofu
za kila siku. Zipo methali zisemazo kikulacho ki nguoni mwako lakini yafaa kwa
hakika kuzichunguza methali za namna hii kabla ya kupokea mafundisho yake.
Zaweza kutufanya tushindwe kuishi vyema na wenzetu.
Copyright
©2013-20202 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment