MASOMO YA MISA, JANUARI
6, 2022
ALHAMISI BAADA YA
EPIFANIA
SOMO 1
1Yoh. 4:19-5:4
Wapenzi: Sisi twampenda
Mungu kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye
anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye
amemwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende
ndugu yake.
Kila mtu aaminiye
kwamba Yesu Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa,
ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twapenda
watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana kila kitu
kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako
ulimwengu, hiyo Imani yetu.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 72:1-2, 14-15 (K)
11
(K) Mataifa yote ya
dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Ee Mngu, mpe mfalme
hukumu yako,
Na mwana wa mfalme haki
yako.
Atawaamua watu wako kwa
haki,
Na watu wako walioonewa
kwa hukumu. (K)
Atawakomboa nafsi zao
na kuonewa na udahlimu,
Na damu yao ina thamani
machoni pake.
Na wamwombee daima;
Na kumbariki mchana
kutwa. (K)
Jina lake na lidumu
milele,
Pindi ling’aapo jua jina
lake liwe na wazao;
Mataifa yote na
wajibariki katika yeye,
Na kumwita heri. (K)
SHANGILIO
Lk. 7:16
Aleluya, aleluya,
Nabii mkuu ametokea
kwetu; na Mungu amewaangalia watu wake.
Aleluya.
INJILI
Lk. 4:14-22
Siku ile, Yesu alirudi
kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za
kandokando. Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu
wote.
Akaenda Nazareti, hapo
alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi
yake, akasimama ilia some. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo,
akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na
kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
Akakifunga chuo,
akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi
wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni
mwenu.
Wakamshuhudia wote,
wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2022, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment