MASOMO YA MISA, JANUARI
5, 2022
JUMATANO BAADA YA
EPIFANIA
SOMO 1
1Yon. 4:11-18
Wapenzi, ikiwa Mungu
alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu
wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, nap endo lake limekamilika
ndani yetu. Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu,
kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. Na sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba
amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa
Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.
Nasi tumelifahamu pendo
alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika
pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Katika hili pendo
limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama
yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu. Katika pendo hamna hofu;
lakini pendo lilio kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na
mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 72:1-2,10,12-13
(K) 11
(K) Mataifa yote ya
ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Ee Mungu, mpe mfalme
hukumu zako.
Na mwana wa mfalme haki
yako.
Atawaamua watu wako kwa
haki,
Na watu wako walioonewa
kwa hukumu. (K)
Siku zake yeye, mtu
mwenye haki atasitawi,
Na wingi wa Amani hata
mwezi utakapokoma
Na awe na enzi toka
bahari hata bahari,
Toka mto hata miisho ya
dunia. (K)
Wafalme wa Tarshisi na
visiwa walete kodi,
Wafalme wa Sheba na
Seba na watoe vipawa.
Naam, wafalme wote na
wamsujudie;
Na mataifa yote
wamtumikie. (K)
Kwa maana atamwokoa
mhitaji aliapo,
Na mtu aliyeonewa iwapo
hana msaidizi
Atamhurumia aliye
dhaifu na maskini,
Na nafsi za wahitaji
ataziokoa. (K)
SHANGILIO
Lk. 4:18-19
Aleluya, aleluya,
Bwana amenituma
kuwahubiri maskini habari njema, na kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.
Aleluya.
INJILI
Mk. 6:45-52
Baada ya watu elfu tano
kula na kushiba, mara Yesu aliwalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani,
watangulie kwenda ng’ambo hata Bethsaidia, wakati yeye alipokuwa akiwaaga
mkutano. Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.
Na kulipokuwa jioni
mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yupo peke yake katika nchi kavu.
Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho;
hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari;
akataka kuwapita. Nao walipomwona anatembea juu ya bahari, walidhani ya kuwa ni
kivuli, wakapiga yowe, kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao,
akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope. Akapanda mle chomboni walimo; upepo
ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao; kwa maana hawakufahamu habari za ile
mikate, lakini mioy yao ilikuwa mizito.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2022, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment