“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba
27, 2021.
------------------------------------------------
JUMATATU,
OKTAVA YA NOELI
Sikuu
ya Yohane, mtume na Mwinjili
Somo
la 1: 1Yn 1: 1-4 Yohane, akiwawakilisha Mitume, anatuambia kwamba msingi wa
kuhubiri kwao ni kwa kitu kile ambacho wameona na kusikia”Neno la uzima”.
Wimbo
wa katikati: Zab 96: 1-2,5-6,11-12 Bwana ni Mfalme, dunia ifurahie, bahari
ishangilie. Furahieni enyi wenye haki katika Bwana, mpeni utukufu wa jina lake.
Injili
Lk 1: 26-38 Yohane anaonesha hali yake yeye na Petro ya kufika kaburi la Yesu
asubuhi siku ya pasaka na kukuta kaburi wazi.
------------------------------------------------
NENO
ALIFANYIKA MWILI KWA AJILI YETU!
Karibuni
sana ndugu zangu wapendwa kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo. Leo ni
sherehe ya Mt. Yohane mtume na Mwinjili. Huyu alikuwa mtume aliyekuwa na
uhusiano wa karibu kabisa na Yesu na Yesu alidiriki hata kumwachia Mama yake
apate kumtunza.
Alipata
kuonyeshwa na Yesu mambo makuu maishani mwake kama tukio la kugeuka sura kwa
Yesu mlimani Tabor. Yeye alisafiri na Yesu hadi akamuona akikata roho juu ya
msalaba. Ukaribu wake na Yesu ulimwezesha kujifunza mengi juu ya Yesu na yote
haya aliyaandika kwenye kitabu chake cha nyaraka tatu.
Kati
ya mitume ni yeye tu aliyebahatika kuishi muda mrefu zaidi, yeye hakuuawa kifo
dini lakini aliteswa sana hadi uzee wake. Kaisari Domisian alimfunga katika
kisiwa cha Patmos na hapo basi aliweza kuandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo
wakristo waliokuwa katika mateso makubwa. Ama kweli alifaulu kulijenga kiimani
kanisa la mwanzo kwa mafundisho yake na ushuhuda wake wa kiimani.
Kwenye
somo la kwanza tunaona akisisitizia jinsi alivyokutana na Yesu, ambaye ni Neno
aliye uzima, Mungu aliyechukua ubinadamu, yeye alipata nafasi ya kumuona,
akamgusa kwa mikono yake mwenyewe na kula naye chakula. Huyu ndiye Yesu. Maneno
haya yalisemwa kuwatia moyo wakristo wachanga ambao walishindwa kuelewa jinsi
Kristo ilivyowezekana kwa Mungu kuzaliwa na kuishi kama mwanadamu. Huyu mtume
anawaambia kwamba iliwezekana kabisa, na sisi wenyewe tulimuona huyu Neno na
tunayo sababu ya kutoa ushuhuda kwa kile tulichokiona.
Hii
ndio imani ya Yohane ndugu zangu. Itusaidie na sisi ambao hadi leo bado
tunajiuliza kama hawa wakristo wa mwanzo-je, iliwezekanaje? Yohane anakueleza
kwamba iliwezekana, yeye mwenyewe aliona kwa macho, akala naye, pia akasikia
sauti ya Mungu toka mbinguni ikisema naye. Sisi tuzidishe imani kwa Yesu, yeye
ndiye neno wa uzima.
Katika
injili, tunaona upendo aliokuwa nao huyu Yohane kwa Yesu, yeye alipopata habari
za ufufuko wa Yesu, alikuwa mwanafunzi wa kwanza kwenda kaburini. Ama kweli
alimpenda Yesu, alijihusisha sana na Yesu, kila mahali alipenda kwenda naye na
ndio maana aliweza kushirikishwa mambo makuu kabisa yamhusuyo Yesu. Sisi
tutembee na Yesu, tupende kusoma Biblia, tusali, tujihusishe na habari zake na
mambo yake yote. Hakika tutaweza kumtambua zaidi, na atakuja kwetu na kujifunua
kwetu.
Yesu
anashindwa kujifunua kwetu kwa sababu habari na stori tunazozipiga kila siku ni
za vijiweni tu, labda ni matusi tu, labda ni kusengenya tu. Stori za namna hii
zinatuzuia kumfahamu Yesu na mwishowe kushindwa kubarikiwa naye. Sisi tutamani
kubarikiwa na Yesu kama Yohane na tangu leo tujihusishe naye, kwa kukaa
mazingira tuwezayo kuongea naye, na maneno tuwezayo kuongea naye.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment