“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba
28, 2021.
------------------------------------------------
JUMANNE,
OKTAVA YA NOELI
Sikukuu
ya Watoto Mashahidi,
Somo
la 1: 1Yn 1:5 – 2:2 Yohana anatuambia kwamba sisi ni wakosefu tunamuhitaji
Kristo. Jitihada yake kubwa ni kutusaidia sisi tuwe mbali na dhambi.
Wimbo
wa Katikati: Zab 123:2-5,7-8 Maisha yetu, kama ndege, yameokoka katika mtego wa
wawindaji, kwani msaada wetu upo katika jina la Bwana aliyeumba mbingu na nchi.
Injili:
Mt 2: 13-18 Mathayo analinganisha kwenda kwa mtoto Yesu Misri na mauaji ya
watoto wachanga-watoto wote wa kiumbe wenye umri chini ya miaka miwili. Hawa
watoto watakatifu waliuwawa kwasababu ya Kristo. Walimfuata Mwanakondoo asiye
na hatia, na kutangaza milele utukufu wa Bwana.
------------------------------------------------
MUNGU
ANAWEZA KUFANYA MAMBO YOTE KUWA MAPYA!
Karibu
ndugu zangu katika adhimisho la misa Takatifu, leo tuna adhimisha sikukuu ya
Watakatifu Watoto Mashahidi: hawa tunasikia habari zao katika injili ya leo.
Wanauawa kwa ajili ya Kristo bila hatia na Herode aliyetaka kulinda ufalme
wake. Mtoto aliyehofiwa alikuwa mmoja tu lakini hofu yake inapelekea kuuawa kwa
watoto wasiofahamu hata maana ya ufalme. Yote haya ni kwa sababu ya uchu wa
madaraka.
Lakini
siku zote uovu hauwezi kuushinda wema. Yesu aliokolewa na kupelekwa Misri na
hivyo ufalme wake ulizidi kubakia. Herode alikufa muda mfupi baadaye na
kupoteza ufalme. Alipokufa alikuta watoto aliowateketeza kama wafalme-mashahidi
mbinguni wakikalia viti kumi na viwili na kuwahukumu makabila yote kumi na
mbili ya Israeli (Mt 19:28). Hivyo, kumshuhudia Yesu hakuna umri, jinsia au
rika. Awe mtoto au mzee anapaswa kumshuhudia Yesu.
Kingine
ndugu zangu nyakati zetu tunaweza kuwa na Maherode wengi wanao winda roho za
watoto wachanga wakiwa tumboni mwa Mama zao na kuwatoa mimba. Yaweza kuwa
wanafanya hivyo kwa hofu ya kuogopa kuitwa Mama au kupoteza uzuri wake kwani
atanyonyesha na watu watafahamu kwamba sasa ana mtoto na hivyo hatapata tena
wanaume wakumpenda. Hawa hawana tofauti sana na Herode, tunaweza kumlaumu
Herodi lakini pengine sisi wenyewe ni Maherode, wale wanaouza dawa za kutolea
mimba, wenye kushauri watu watoe mimba, wazazi wanaotoa mimba kisa eti mtoto
amekuja wakati ambao sio wenyewe, hatuna tofauti na Herode.
Tutetee
watoto wachanga tangu akiwa tumboni mwa mama yake, hatuwezi kusema sisi tupo
huru kuangamiza maisha ya wengine. Hakuna Mwanadamu aliyepewa uhuru wa namna
hii. Ni Mungu mwenyewe mwenye kuleta uhai na mwenye mamlaka ya kuuchukua. Kama
tumefanya hivi tuache na kumrudia Mungu.
Pia
tusi waangamize wenzetu kwa hofu ya kuogopa kupoteza umaarufu wetu. Tusiogope
kujiunga nao watufundishe.Tukiwa katika nia hii, tuenende katika nuru yake na
tuziungame na kuzisafisha dhambi zetu kwa damu yake, kama tunavyoambiwa katika
somo la kwanza.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment