MASOMO
YA MISA, DESEMBA 27, 2021
SIKUKUU
YA MT. YOHANE, MTUME NA MWINJILI
SOMO
1
1Yoh.
1:1 – 4
Lile
lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu,
tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; (na
uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule
uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu; hilo tuliloliona na
kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na
ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. Na haya
twayaandika, ili furaha yetu itimizwe.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
97:1 – 2, 5 – 6, 11 – 12 (K) 12
(K)
Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana.
Bwana
ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa
vingi na vifurahi.
Mawingu
na giza vyamzunguka,
Haki
na hukumu ndio msingi wa kiti chake. (K)
Milima
iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,
Mbele
za Bwana wa dunia yote.
Mbingu
zimetangaza haki yake,
Na
watu wote wameuona utukufu wake. (K)
Nuru
imemzukia mwenye haki,
Na
furaha wanyofu wa moyo.
Enyi
wenye haki, mfurahieni Bwana,
Na
kulishukuru jina lake takatifu. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya Mitume inakusifu.
Aleluya.
INJILI
Yn.
20:2 – 8
Siku
ya kwanza ya juma, Mariamu Mgdalena alikwenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na
kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa
Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.
Basi
Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini.
Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi
kuliko Petro, akawa wa kwanza wa kufika kaburini. Akainama na kuchungulia,
akaviona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia.
Basi
akaja na Simoni Petro akimfuata, akaingiza ndani ya kaburi; akavitazama
vitambaa vilivyolala; na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja
na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake. Basi ndipo
alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika
kaburini, akaona na kuamini.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment