MASOMO
YA MISA, DISEMBA 7, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
40:1 – 11
Watulizeni
mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa
Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake
umeachiliwa, kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi
zake zote.
Sikiliza
ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana, nyosheni jangwani
njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, na kila mlima na kilima
kitashushwa; palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa.
Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja, kwa kuwa
kinywa cha Bwana kimenena haya.
Sikiliza,
ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani,
na wema wake wote ni kama ua la kondeni. Majani yakauka, ua lanyauka, kwa
sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani. Majani
yakauka, ua lanyauka, bali neon la Mungu wetu litasimama milele.
Wewe
uuhubiriye Sayuni habari njema, panda juu ya mlima mrefu; wewe uuhubiriye
Yerusalemu habari njema, paza sauti kwa nguvu. Paza sauti yako, usiogope;
iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu! Tazameni, thawabu yake I pamoja
naye, na ijara yake I mbele zake. Atalilisha kundi lake kama mchungaji,
atawakusanya wanakondoo mikononi mwake; na kuwachukua kifuani mwake, nao
wanyonyeshao atawaongoza polepole.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
96:1 – 3, 10 – 13 (K) Isa. 40:9 – 10
(K)
Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Mwimbieni
Bwana, nchi yote.
Mwimbieni
Bwana likarikini jina lake,
Tangazeni
wokovu wake siku kwa siku. (K)
Wahubirini
mataifa habari za utukufu wake,
Na
watu wote habari za maajabu yake.
Semeni
katika mataifa, Bwana ametamalaki,
Atawahukumu
watu kwa adili. (K)
Mbingu
na zifurahi, nchi na ishangilie,
Bahari
na ivume na vyote viijazavyo.
Mashamba
na yashangilie, na vyote vilivyomo,
Ndipo
miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha. (K)
Mbele
za Bwana, kwa maana anakuja,
Kwa
maana anakuja aihukumu nchi,
Atahukumu
ulimwengu kwa haki,
Na
mataifa kwa uaminifu wake. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Siku
ya Bwana i karibu, Tazama atakuja kutuokoa.
Aleluya.
INJILI
Mt.
18:12 – 14
Siku
ile, Yesu aliwaambia wafuasi wake. Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja
akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta
yule aliypotea? Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahi huyo Zaidi,
kuliko wale tisa na tisini wasiopotea.
Vivyo
hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa
apotee.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment