MASOMO
YA MISA, DISEMBA 17, 2021
IJUMMA,
JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO
1
MWA.
49:2, 8 – 10
SIKU
ILE, Yakobo aliwaita wanawe, akawaambia: Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa
Yakobo, msikilizeni Israeli, baba yenu.
Yuda,
ndugu zako watakusifu, mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba
yako watakuinamia. Yuda ni mwanasimba, kutoka katika mawindo, mwanangu,
umepanda; aliinama akajilaza kama simba, na kama simba, na kama simba mke; ni
nani atakayemwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, wala mfanya sharia
kati ya miguu yake, hata atakapokuja yeye, mwenye milki, ambaye mataifa
watamtii.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
72:1 – 4, 7 – 8, 17 (K) 7
(K)
Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, na wingi wa amani hata mwezi
utakapokoma.
Ee
Mungu, mpe mfalme hukumu zako,
Na
mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua
watu wako kwa haki,
Na
watu wako walioonewa kwa hukumu. (K)
Milima
itawazalia watu Amani,
Na
vilima navyo kwa haki.
Atawahukumu
walioonewa wa watu,
Atawaokoa
wahitaji, atamseta mwenye kuonea. (K)
Siku
zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na
wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.
Na
awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka
Mto hata miisho ya dunia. (K)
Kwa
maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na
mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.
Atamhurumia
aliye dhaifu na maskini,
Na
nafsi za wahitaji ataziokoa. (K)
Jina
lake na lidumu milele,
Pindi
ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa
yote na wajibariki katika yeye,
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Hekima ya Aliye juu, unayepanga yote kwa nguvu zako na utaratibu mwema, uje
kutufunza njia ya busara.
Aleluya.
INJILI
Mt.
1:1 – 17
Kitabu
cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
Ibrahimu
akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na zera kwa Tamari; Peresi
akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu
akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu;
Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; Yese akamzaa mfalme Daudi.
Daudi
akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria; Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu
akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa
Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi
akamzaa Hezekia; Hezekia akamzaa Manase; Manase akamaza Amoni; Amoni akamzaa
Yosia; Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
Na
baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa
Zerubabeli; Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu
akamzaa Azori; Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa
Eliudi; Eliudi akamzaa Eleazari; eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa
Yakobo.
Yakobo
akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa Yesu aitwaye Kristo.
Basi
vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi
hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa
Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Bwana.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment