MASOMO
YA MISA, DESEMBA 14, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO
1
Sef.
3:1 – 2, 9 – 13
Bwana
asema: Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! Hakuitii
sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini Bwana; hakumkaribia Mungu wake.
Maana
hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la
Bwana, wamtumikie kwa nia moja. Maana toka nchi iliyo mbali na mito ya kuishi;
waniombao dua, yaani, binti za watu wangu waliotawanyika, wataleta matoleo
yangu.
Siku
ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu
wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika
mlima wangu mtakatifu. Lakini nitasaza ndani yako watu walioonewa na maskini
nao watalitumainia jina la Bwana. Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala
kusema uo0ngo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; kwa maana
watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
34:1 – 2, 5 – 6, 16 – 17, 18, 22 (K) 6
(K)
Maskini aliita, Bwana akasikia.
Nitamhimidi
Bwana kila wakati,
Sifa
zake zi kinywani mwangu daima.
Katika
Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu
wasikie wafurahi. (K)
Wakamwelekea
macho wakati wa nuru,
Wala
nyuso zao hazitaona haya.
Masikini
huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa
na taabu zake zote. (K)
Uso
wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe
kumbukumbu lao duniani.
Walilia,
naye Bwana akasikia,
Akawaponya
na taabu zao zote. (K)
Bwana
yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na
waliopondeka roho huwaokoa.
Bwana
huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala
hawatahukumiwa wote wamkimbiliao. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Uje,
Bwana, wala usikawie; Uzisamehe dhambi za taifa lako.
Aleluya.
INJILI
Mt.
21:28 – 32
Siku
ile, Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee: Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na
wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye
kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.
Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki;
baadaye akatubu, akaenda. Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye?
Wakamwambia, Ni yule wa pili.
Basi
yesu akawaambia, Amin, nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele
yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu Yohane alikuja kwenu kwa njia
ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini; nanyi
hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment