MASOMO
YA MISA NOVEMBER 12, 2021
IJUMAA
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
Hek.
13:1-9
Bila
shaka wanadamu wote kwa asili ni ubatili, ambao hawana akili za kumtambua
Mungu; tena hawakupata uwezo wa kumjua Yeye aliopo kwa kuvitazama viumbe vizuri
vinavyoonekana, wala kwa kuyaangalia yaliyofanywa hawakufahamu yule Fundi
aliyeyafanya. Walakini moto, ama upepo, ama hewa nyepesi, ama mzunguko wa
nyota, ama mafuriko ya maji, ama mianga ya mbinguni, walidhania kuwa ni miungu
inayoutawala ulimwengu!
Huenda
ilikuwa kwa kupendezwa na uzuri wake walivyodhania viumbe hivyo kuwa ni miungu,
basin a wajue kadiri gani Bwana, Mfalme wao, avipatavyo; kwa maana Yeye aliye asili
ya uzuri ndiye aliyeviumba.
Lakini
kama ilikuwa kwa kuzistaajabia nguvu zake na maongozi yake, na wafahamu kwa
kuviangalia kadiri gani Yeye aliyeviumba anayo nguvu zaidi; maana kwa jinsi
uzuri hata wa viumbe vilivyoumbwa ulivyo mkuu, kwa kadiri iyo hiyo mwanadamu
huyatunga mawazo yake juu ya Muumba.
Walakini
watu hao hawana hatia nyingi. Madhali yawezekana kwamba hao wamekosea tu, pindi
wanapomtafuta Mungu, na kutamani kumwona; kwa sababu huishi katikati ya viumbe
vyake, huvichunguza kwa bidi, na mwisho hujitoa kwa maono yao, mradi vitu
vyenyewe wanavyovitazama ni vizuri kweli kweli.
Walakini
tena watu hao hawana udhuru. Kwa maana wakiwa walikuwa na uwezo wa kufahamu
kadiri hiyo, hata kuweza kuchungulia taratibu ya viumbe, imekuwaje ya kwamba
hawakudiriki upesi kutambua Mfalme Mkuu wa viumbe hivyo vyake?
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:1-4 (K) 1
(K)
Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu.
Mbingu
zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na
anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Mchana
husemezana na mchana,
Usiku
hutolea usiku maaarifa. (K)
Hakuna
lugha wala maneno,
Sauti
yao haisikilikani.
Sauti
yao imeenea duniani mwote,
Na
maneno yao hata miisho ya ulimwengu. (K)
SHANGILIO
Zab.
111:7,8
Aleluya,
aleluya,
Maagizo
yako yote, Ee Bwana, ni amini, yamethibitika milele na milele.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:26-37
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa
katika siku zake Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na
kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka
ikawaangamiza wote. Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa
wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini
siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulikunya moto na kibiriti kutoka mbinguni
vikawaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana
wa Adamu.
Katika
siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili
kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma. Mkumbukeni mkewe Lutu.
Mtu yeyote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na yeyote
atakayeiangamiza ataiponya. Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika
kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa
wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
Wakajibu,
wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia. Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced
by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment