“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakri
ya kila siku
Ijumaa,
Novemba 12, 2021,
Juma
la 32 la Mwaka
Hek
13: 1-9;
Zab
19: 1-4 (K) 1;
Lk
17: 26-37.
KUKABIDHI
MAISHA YETU KWA MUNGU!
Karibuni
wapendwa kwa adhimisho la Misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la Bwana katika
asubuhi ya leo tukianza kwa kuliangalia somo la kwanza. Hapa tunamkuta
mwandishi akiwalaumu wale ambao katika jamii yake walionekana kama wataalamu wa
mambo, kama wajuzi na waliheshimika na kila mtu. Hawa waliweza kufanya utabiri
wa vitu vingi, kutibu hata magonjwa makubwa, kuongea maneno ya kuvutia watu
sana. Lakini cha ajabu ni kwamba walishindwa kumwona Mungu katika viumbe vyake,
walishindwa kujua kwamba viumbe vinatangaza utukufu wa Mungu kama tunavyoelezwa
katika zaburi ya wimbo wa katikati. Hili walishindwa ndugu zangu.
Sasa
mwandishi wa kitabu hiki anashangaa kwani watu hawa bado ndio wanaonekana
kwamba wana hekima, kama waheshimiwa lakini ki ukweli hakuna kitu kabisa. Hawa
watu ni sifuri kabisa.
Somo
la injili ni mwendelezo wa maada kama hii. Hapa tunakuta tena habari juu ya
watu wanavyokosa kuwa na hekima, tena ni wale ambao katika jamii wanaonekana
kama wajanja. Injili inatuambia kwamba hawa ndio wanaoongoza kwa kukosa hekima
na katika kila dhoruba wanakamatwa. Kwa mfano katika ile dhoruba ya Nuhu, Nuhu
alionekana kama kachanganyikiwa, kama aliyekosa kazi na hakuna aliyemsikiliza.
Wale wajanja ndio walionekana kuwa watu. Lakini dhoruba imekuja, wamekamatiwa
huko na kufa wote. Na siku za ujio wa pili wa Masiha Yesu anasema kwamba
zitakuwa hivyo hivyo, kutakuwa na aina za watu, wale wanaojiona wajanja, wenye
hekima watakamatwa kama ilivyokuwa siku za Nuhu.
Ndugu
zangu, masomo yetu ya leo yanatuambia kwamba tutumie hekima zetu vizuri
tukijiandaa kwa ujio wa pili. Usiridhike ukiona kwamba unaitwa bosi bosi, wewe
unajua habari yote ya mjini, wewe kila sherehe unaalikwa, wewe ni maarufu,
kanisani unaitwa kama kamheshimiwa halafu ufikiri kwamba umesha ipata mbingu.
Tulia ndugu yangu. Fikiria maisha yako. Angalia ni nani anayekuita mjanja.
Unaweza kukuta unaitwa na wezi wenzako kwamba wewe ni mjanja na kichwa
kikavimba na kujisahau na kuona kwamba wewe ni kila kitu. Angalia utashangaa mwenzako
anatwalia na wewe waachwa.
Kingine
ni juu ya toba. Kwa kweli toba inaokoa. Anayefanya toba hataachwa na Mungu hata
siku moja. Tukifanya toba kwa nguvu zote, nakwambia Mungu haachagi kabisa,
haachagi mtu yoyote. Tumesikia kwamba wako watu wawili wamelala lakini mmoja
atatwaliwa. Kwa kweli anayefanya toba atatwaliwa tu. Mungu hatamwacha. Hii ni
kwa sababu Mungu ni mwenye huruma nyingi mno na kila afanyaye toba atabahatika
kumwona. Hivyo, tunapojiandaa kwa ujio wa pili, toba ni muhimu.
Ukisoma
kitabu cha Ufunuo, sura ya tatu, utatambua kwamba Yesu analiagiza kila kanisa
lililo na dhambi kwamba litubu. Tutubu jamani.
Kila
mtu anadhambi zake jamani. Wengine tumewaonea wenzetu kazini, tumewasengenya,
tumewafanya wenzetu wachukiwe na wengine, tumewaonea wafanyakazi wetu wa ndani,
tumekataa kuwatunza wazazi wetu, huku tukijitamba mjini kwamba tuna fedha na
kusifiwa na watu na kuonekana wenye hekima, wakati wazazi kijijini au nyumbani
wanakufa njaa. Tuache maisha hayo nakuanza ukurasa mpya leo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment