MASOMO YA MISA NOVEMBA 27, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Dan.
7:15-27
Mimi
Danieli, roho yangu ilihuzunika mwilini mwangu, na hayo maono ya kichwa changu
yakanifadhaisha. Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza
maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo
hayo. Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wane watakaotokea duniani. Lakini
watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele,
naam hata milele na milele.
Kisha
nalitaka kujua maana ya yule mnyama wanne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote,
mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya
shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu
yake; na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe
nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile
yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari
kuliko wenzake. Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu,
ikawashinda; hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake. Aliye juu
wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.
Akanena
hivi, Huyo mnyama wanne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali
na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande
vipande. Na habari za zile pembe kumi katika ufalme huo wataondoka wafalme
kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza;
naye atawashusha wafalme watatu. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu,
naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na
sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu
wakati. Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuyapoteza na
kuyaangamiza, hata milele. Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya
mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme
wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Dan.
3:82-87 (K) 59
(K)
Msifuni na mwadhimisha milele.
Wanadamu,
mhimidi Bwana;
Msifuni
na kumwadhisha milele.
Bani
Israeli, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Makuhani
wa Bwana, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Watumishi
wa Bwana mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Roho
na nafsi zao wenye haki mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Watakatifu
na wanyenyekevu moyoni,
Mhimidini
Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
SHANGILIO
Yak.
1:18
Aleluya,
aleluya,
Kwa
kupenda kwake mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko
la viumbe vyake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:34-36
Yesu
aliwambia wanafunzi wake: Jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na
ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego
unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia
nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo
yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
No comments:
Post a Comment