“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila kila siku
Jumamosi,
Novemba 27, 2021.
Juma
la 34 la Mwaka
Jumamosi,
kumbukumbu ya Bikira Maria
Dan
7: 15-27;
Dan
3: 82-87 (R) 59;
Lk
21: 34-36.
KUKUTANA
NA MUNGU KATIKA KILA HALI YA MWANADAMU
Leo
ni siku ya mwisho katika mwaka wa Liturjia ya mwaka huu. Kesho tunaanza kipindi
cha majilio. Mara nyingi Kanisa linaelekeza mambo ya mwisho na mwisho wa maisha
yetu hapa duniani. Ni mwaliko kwa waamini kuwa tayari kwa ajili ya mwisho wa
ulimwengu. Somo la kwanza linaangalia ni kwa jinsi ghani Watakatifu wa Mungu
watakavyo pambana na magumu na changamoto za mwisho wa nyakati, wakati Injili
ikituambia kwamba mwisho wa nyakati upo kati yetu kila wakati.
Nabii
Danieli anaona ndoto juu ya wanyama wanne. Danieli aliogopeshwa sana na maono
haya. Lakini mwishoni anatambua kwamba hakuna mnyama ambaye anaweza kuishi
milele.bali utukufu wa mwisho unapewa kwa watakatifu wa Mungu.
Madhulumu
kutoka kila mahali haina maana tumeacha neema ya Mungu. Mapingano hayo na
ufalme wa Mungu yataendelea mpaka mwisho wa nyakati. Mtakatifu Yohane wa
Msalaba alisema kuna maadui watatu ambao tutakutana nao wakati tukisonga mbele
kwenda kwenye ukamilifu: shetani, dunia na mwili wetu. Maisha ya mwanadamu
yanapaswa kuishia na kuona uso wa Mungu. Na hili ndilo linalopaswa kuwa lengo
letu. Hivyo kila mmoja wetu lazima akumbane na adui mmoja wapo katika safari
yake.
Yesu
anatuambia kwamba tunapaswa kuwa makini. Muda mwingi nguvu zetu zinaishia
katika hofu. Kwasababu hatuwezi kutabiri kuhusu wakati ujao tunaishi kuwaza
mambo mengi na yasio tusaidia kukuwa kiroho. Badala yake tunapaswa kuongozwa na
sala kama silaha yetu katika safari yetu ya hapa duniani. Na hili litafanya
safari yetu kuwa ya Amani.
Injili
inatuambia kuhusu kukutana na Mwana wa Mungu. Kwanini? Kwasababu yeye ni Bwana
wetu, rafiki, zaidi ya yote ni Upendo wetu. Wale wote ambao watamshinda adui
watasimama mbele ya Mungu na kumsifu bila mwisho na kumtolea yeye sifa. Ni
furaha iliojee!
Sala:
Bwana, ninakupenda wewe Bwana na ninatamani kukupenda wewe zaidi ya yote.
Nisaidie mimi niweze kusimama imara katika maisha yangu ya Imani. Nisaidie
kukaza macho yangu kwako na kujiandaa utakapo kuja. Ninakuomba nijiandae kwa
sala na fadhila, wakati nitakapo kutana na uso wako. Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment