MASOMO YA MISA NOVEMBA 23, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Dan.
2:31-45
Danieli
alimwambia Nebukadreza: Wewe, Ee mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana.
Sanamu hii, ilivyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama
mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii, kichwa chake
kilikuwa ni cha dhahabu safi, kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo
lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu
yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila
kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma
na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo na ile
shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja, vikawa
kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha, hata
pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa mlima
mkubwa, likaijaza dunia yote.
Hii
ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. Wewe, Ee
mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na
nguvu, na utukufu; na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege
wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe, u
kichwa kile cha dhahabu.
Na
baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala
dunia yote. Na ufalme wan ne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma
huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote,
ndivyo utakavyovunjavunja na kuseta. Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za
miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule
utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama
vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. Na kama vidole
vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa
nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. Na kama vile ulivyokiona kile
chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu
za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na
udongo.
Na
katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao
hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja
falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na
ya kuwa lilivunjwavunjwa kile chuma, na ile shaba, na ule udongo, na ile fedha,
na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa
baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Dan.
3:57-61 (K) 59
(K)
Msifuni Bwana na kumwadhimisha milele.
Enyi
viumbe vyote vya Bwana mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Malaika
za Bwana, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Enyi
mbingu, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Maji
yote yaliyo juu angani, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Mawezo
yote ya Bwana, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
SHANGILIO
Yak.
1:18
Aleluya,
aleluya,
Kwa
kupenda kwake mwenye, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko
la viumbe vyake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:5-11
Watu
wa kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa
kwa mawe mazuri na sadaka za watu, Yesu alisema, Haya mnayoyatazama, siku
zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Wakamwuliza
wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo
hayo ya karibu kutukia?
Akasema,
Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu,
wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao. Nanyi
mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi
kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi. Kisha aliwaambia, Taifa
litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na
matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha
na ishara kuu kutoka mbinguni.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reprod
No comments:
Post a Comment