MASOMO
YA MISA NOVEMBA 2, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 31 LA MWAKA WA KANISA
KUWAKUMBUKA
WAAMINI MAREHEMU WOTE
SOMO
1
Ayu.
19:1,23-27
Laiti
maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni! Yakachorwa katika
mwamba milele, kwa kalamu ya chuma na risasi. Lakini mimi najua ya kuwa
Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya
ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;
Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.
Mtima wangu unazimia ndani yangu!
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
23 (K) 1
(K)
Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Bwana
ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa
na kitu.
Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza.
Kando
ya maji ya utulivu huniongoza. (K)
Hunihuisha
nafsi yangu; na kuniongoza,
Katika
njia za haki kwa ajili ya jjina lake.
Naam,
nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa
mabaya;
Kwa
maana wewe upo pamoja name,
Gongo
lako na fimbo yangu vyanifariji. (K)
Waandaa
meza mbele yangu,
Machoni
pa watesi wangu.
Umenipaka
mafuta kichwani pangu,
Na
kikombe changu kinafurika. (K)
Hakika
wema na fadhili zitanifuata,
Siku
zote za maisha yangu;
Nami
nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SHANGILIO
Ufu.
14:13
Aleluya,
aleluya,
Heri
wafu wafao katika Bwana tangu sasa! Wapate kupumzika baada ya taabu zao, kwa
kuwa matendo yao yafuatana nao.
Aleluya.
INJILI
Mt.
5:1-12
Yesu
alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake
walimjua; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
Heri
walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni;
Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye
njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao
watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri
wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya
haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri
ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa
ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni;
kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment