“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne,
Novemba 2, 2021,
Juma
la 31 la Mwaka wa Kanisa
Marehemu
Wote
Is
29:6-9;
Zab
22;
Rom
5:5-11;
Mt.
5:1-12
MIMI
NI UFUFUO NA UZIMA!
Leo
Kanisa Katoliki linawaombea watoto wake, ambao katika siku ya kufa, japo
walitamani utukufu usio na mwisho Mbinguni, hawakuwa wamejiandaa vyema kuingia
katika furaha hiyo na pia hawastahili kwenda motoni. Hawa ni roho zilizoko
twaharani- ambao wanatakaswa ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni. Lakini pia
sisi tujifunze kitu kwamba kila mmoja wetu amesogea siku moja kuelekea kifo. Ni
njia yetu wote.
Sala
kwa ajli ya marehemu zilianza na Wakristo wa kwanza, mwanzoni kabisa, kuwaombea
mashahidi wa kwanza. Walifanya hivyo kumshukuru Mungu mwenyenzi kwa ajili ya
mashahidi wa kwanza kwa ujasiri wao, na zaidi sana kwa Imani yao. Walifanya
hivyo kwasababu walitambua kifungo kisichoweza kuvunjwa kinacho tuunganisha
sisi ndani ya Kristo, walio hao na waliokufa pia. Kifo hakiwezi kuvunja na
kutenga familia ya Kristo, hakiwezi kuharibu umoja na muunganiko wetu tunao
shiriki katika Kristo sisi zote kama tupo hapa duniani au tumeenda katika
maisha yajayo.
Kuwaombea
wafu ina msingi wake katika maandiko matakatifu “na hivyo (Yuda Wamakabayo)
akafanya maombi kwa ajili ya kuwaombea wale waliokufa, ili wasamehewe dhambi zao”
(2 Mak 12:46). Kuanzia mwanzoni, Kanisa limeheshimu kuwakumbuka marehemu na
kutolea sala kwa ajili yao, na juu ya yote sadaka ya Ekaristi, ili waoshwe,
waweze kupata heri ya mwanga wa Mungu. Kanisa pia linahimiza kutolea sadaka,
rehema, na kazi za toba kwa niaba ya marehemu (KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI,
1032).
Lakini
hata tungekuwa na ujasiri namna ghani na hata tukipokea ukweli katika hali ya
chanya, siku ya kuiacha dunia hii haieleweki na ni lazima, kwasababu kunakuwepo
na utengano wa mwili na roho. Hivyo Kanisa linatuhimiza kila mara kujiandaa
wenyewe kila mara kwa saa ya kufa kwetu.
Sala:
Mungu mwenye nguvu na huruma, umefanya kifo kiwe mlango wakuingia uzima wa
milele. Uwatazame kwa huruma ndugu zetu marehemu, wafanye wawe pamoja na Mwanao
kwa mateso na kifo, ili, wakiwa wamefunikwa na damu ya Kristo, waweze kuja
mbele zako wakiwa huru kutoka katika dhambi. Amina.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment