MASOMO YA MISA NOVEMBA 17, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 33 LA MWAKA
SOMO
1
2
Mak. 7:1,20-31
Ilitokea
ya kuwa ndugu saba, pamoja na mama yao, walikamatwa kwa amri ya mfalme na
kuteswa sana kwa mijeledi na mapigo ili kuwashurutisha kuonja nyama marufuku ya
nguruwe.
Aliyekuwa
wa ajabu hasa, na kustahili kumbukumbu la heshima, ndiye yule mama. Maana aliwaona
wanawe saba wakifa kwa siku moja, akistahimili kwa moyo thabiti kwa ajili ya
matumaini aliyoyaweka kwa Bwana. Kwa roho hodari aliimarisha tabia yake ya kike
kwa ushupavu wa kiume, akamfariji kila mtoto kwa lugha ya wazee wao, akisema,
Jinsi mlivyoingia tumboni mwangu sijui. Si mimi niliyekupeni roho na uzima,
wala si mimi niliyeziunga sehemu za miili yenu. Bali ni yeye, Muumba ulimwengu;
yeye aumbaye wanadamu na kukikusudia chanzo cha vitu vyote; naye kwa rehema
zake akakurudishieni roho zenu na uzima wenu, kwa kuwa ninyi sasa mnajihesabu
kuwa si kitu kwa ajili ya amri zake.
Antioko
alijiona anafedheheshwa, lakini bila kuangalia mzaha wa maneno yake, alimsihi
yule mdogo, maana alikuwa yungali hai,
akamwambia, si kwa maneno tu ila pia kw auapa, ya kuwa, akama ataziacha sheria
za wazee wake, atampatia mali nyingi na hali njema; tena, atamfanya mmoja wa
rafiki zake na kumkabidhi kazi za ufalme. Yule kijana asipokubali, alimwita
mama yake, akamtaka amshawishi mtoto ajiokoe. Akasema naye kwa maneno mengi,
hata mwisho alikubali kumshauri mwanawe.
Akamwinamia
na huku anamdhihaki yule mfalme mkali akasema hivi kwa lugha ya wazee wake:
Mwanangu, unirehemu mimi niliyekuchukua tumboni mwangu kwa miezi tisa, na
kukutunza na kukulea mpka sasa. Nakusihi, mwanangu, inua macho yako utazame
mbingu na nchi, ukaone vitu vyote vilivyomo; fahamu kwamba Mungu hakuviumba kwa
vitu vilivyokuwapo. Na ndivyo alivyofanya wanadamu pia. Usiogope mwuaji huyu;
jionyeshe umestahilika sawasawa na dnugu zako. Kubali kufa kwako, ili kwa
rehema ya Mungu nikupokee tena pamoja na ndugu zako. Hakudiriki kuyamaliza
maneno yake, ila yule kijana alisema, Mnamngoja nini? Mimi siitii amri ya
mfalme, bali naitii amri ya sheria waliyopewa baba zetu kwa Musa. Wewe,
uliyebuni kila namna ya uovu juu ya Waebrania, hutaokoka kabisa katika mikono
ya Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
17:1,5-6,8,15 (K) 15
(K) Nishibishe kwa sura yako, Ee Bwana.
Ee
Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu,
Utege
sikio lako kwa maombi yangu,
Yasiotoka
katika midomo ya hila. (K)
Nyayo
zangu zimeshikamana na njia zako,
Hatua
zangu hazikuondoshwa.
Ee
Mungu, nimekuita kwa maana utaitikia,
Utege
sikio lako ulisikie neno langu. (K)
Unilinde
kama mboni ya jicho,
Unifiche
chini ya uvuli wa mbawa zako.
Nikutazame
uso wako katika haki,
Niamkapo
nishibishwe kwa sura yako. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Lk.
19:11 – 28
Makutano
waliposikia, Yesu aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na
Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara. Basi
akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie
ufalme na kurudi. Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya
fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. Lakini watu wa mji wake
walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
Ikawa
aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha,
ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. Akaja wa kwanza, akasema,
Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. Akamwambia, Vema,
mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na
mamlaka juu ya miji kumi. Akaja wa pili, akasema, Bwana fungu lako limeleta
mafungu matano faida. Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
Akaja
mwingine akasema, Bwana hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika
leso, Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna
usichopanda. Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako mtumwa mwovu wewe.
Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na
faida yake? Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe
yule mwenye mafungu kumi. Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi, Nawaambia,
Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho
nacho.
Tena,
wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwanchinje mbele yangu.
Na
laipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
No comments:
Post a Comment