MASOMO
YA MISA NOVEMBA 11, 2021
ALHAMISI
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
Hek.
7:22-8:1
Mradi
ndani yake mna roho ya welekevu, takatifu, ya pekee, yenye namna mbalimbali,
iliyoerevuka, nyepesi kuenea, Dhahiri kusema, safi, wazi, isiyoharibika, ya
kupenda wema, hodari, bila kuzuiwa, yenye ukarimu, ya kupenda wanadamu,
thabiti, amini, bila mashaka, yenye nguvu, yenye kuangalia mambo yote, na
kuingiliana na roho zote zilizo na welekevu, zilizo safi, zilizoerevuka sana.
Kwa sababu Hekima huenda upesi kila upande hata kupita mwendo wowote, naam,
huenea kote kote katika mambo yote na kupenya ndani yake kwa ajili ya usafi
wake.
Maana
ndiyo pumzi ya uwezo wa Mungu, na miminiko nakawa la utukufu wake Mwenyezi,
hivyo lolote lililo najisi haliwezi kuingia ndani yake. Ndiyo mwangaza kutoka
kwa nuru ya milele, na kioo kisicho na mawaa cha kutenda kwake Mungu, na mfano
wa wema wake. Nayo ni moja, ina uwezo wa kutenda yote; hujikalia, huweza
kuhuisha yote; na tangu kizazi hata kizazi huwaingilia roho takatifu, huwafanya
wanadamu kuwa rafiki za Mungu na manabii; maana Mungu humpenda yeye tu akaaye
na Hekima. Marini kuliko jua. Hekima hupita makundi ya nyota; ikilinganishwa na
nuru, huonekana ya kuwa imezidi; mradi baada ya nuru ya mchana hufuata usiku,
bali juu ya Hekima hakuna ovu liishindalo.
Hekima
huenea kwa nguvu nyingi toka pembe hii hata pembe hii ya dunia, na
kuyaratibisha mambo yote kwa jinsi ya kufaa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
119:89-91,130,135,175 (K) 89
(K)
Ee Bwana, neno lako lasimama hata milele.
Ee
Bwana, neno lako lasimama,
Imara
mbinguni hata milele.
Uaminifu
wako upo kizazi baada ya kizazi.
Umeiweka
nchi, nayo inakaa. (K)
Kwa
hukumu zako vimesimama imara hata leo,
Maana
vitu vyote ni watumishi wako.
Kufafanusha
maneno yako kwatia nuru,
Na
kumfahamisha mjinga. (K)
Umwangazie
mtumishi wako uso wako,
Na
kunifundisha amri zako.
Nafsi
yangu na iishi, ipate kukusifu,
Na
hukumu zako zinisaidie. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:135
Aleluya,
aleluya,
Umwangazie
mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:20-25
Yesu
alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia,
Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au,
kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Akawaambia
wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana
wa Adamu, msiione. Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke
mahali mlipo, wala msiwafuate; kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande
huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana
wa Adamu katika siku yake. Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na
kukataliwa na kizazi hiki.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment