“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Novemba 11, 2021.
Juma
la 32 la Mwaka
Hek
7: 22 – 8: 1;
Zab
119: 89-91, 130, 135, 175 (K) 89;
Lk
17: 20-25.
UFALME
WA MUNGU KATI YETU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza. Hapa tunakutana na fundisho juu ya
hekima na hekima hii inavyoelezewa na tabia zake ama kweli ni hekima ya ajabu.
Tunaambiwa kwamba ina nguvu ajabu, yaenea pande zote za dunia, yaweza kufanya
upya vitu vyote, ndiyo inayowafanya watu wawe marafiki wa Mungu, inanguvu na
yapita roho zote. Hii ndiyo hiyo hekima ndugu zangu.
Katika
wimbo wa katikati, hekima hii inafananishwa na neno la Mungu. Hili ndilo lenye
nguvu ya kutenda kama hii hekima hii tuliyoisikia katika somo la kwanza. Ndugu
zangu hekima hii ni kitu gani? Ni Roho wa Mungu ndugu zangu. Unapo mchagua
Mungu kuwa Baba yako, Roho yake huja na kukaa ndani yako, na kukuongoza namna
ya kutenda. Ndio hii Roho ya Bwana ndugu zangu ifanyayo kazi ndani yako na hii
ndiyo hekima yenyewe ndugu zangu. Na katika neno la Mungu hii hekima hupatikana
kama tulivyosikia katika wimbo wa katikati kwani neno la Mungu lina Roho tena
ni uzima. Neno la Mungu lenyewe limesheehini Roho ya Bwana, limebeba Roho yake
ndugu zangu. Neno hili ni hekima kwani laweza kumwongoza mwanadamu katika
maisha ya umilele.
Na
hii ndiyo hekima inayopaswa ituongoze katika siku za mwisho wakati wa ujio wa
utawala wa Mungu kama tunavyosikia katika injili ya leo. Hii ni kwa sababu
utawala wa Mungu utakuja bila kutabirika na cha ajabu utawala huo Yesu anasema
upo kati yetu tayari yaani yeye mwenyewe ndio huo utawala. Uwepo wake unatakiwa
uchukuliwe kama sehemu yetu sisi ya kukesha kila wakati, kutokutumia muda wetu
vibaya, kwani hakutakuwa na wa kutoa matangazo kama ya harusi au kipaimara ati
yakitangaza ati ufalme wa Mungu umeshakuja. Kinachotakiwa ni kukesha na ile
hekima ya Kimungu, kama tunayo ndiyo itakayotusaidia kuelewa hili. Kama hatuna
hii hekima, nakwambia hatutaweza kabisa kufanya hili. Tutajikuta tunayumbishwa
yumbishwa huko na huko kama makapi yapeperushwayo na upepo. Hekima hii ndiyo
itakayotusaidia. Tusipokuwa na hekima tutakuwa tunayumbishwa na waalimu wa
uongo.
Hivyo
ndugu zangu tukazane kuomba hii hekima itusadie ili tupambane na dhoruba kama
hizi tulizozisikia katika injili. Hekima hii tutaipata kwa kusoma neno la
Mungu, kusali kila siku, kuungama na kutenda matendo mema. Ukifanya hivi, Roho
wa Bwana anakuja na kukaa kati yako na kutenda pamoja nawe na kukuongoza mbele.
Anakupatia nguvu ya kupambana na dhoruba mbalimbali za kimaisha. Unaepuka kuwa
kama makapi. Ukiendekeza ulevi, masengenyo nakwambia hutaipata hekima hii.
Kingine
ndugu yangu, ni kwamba injili ya leo inatuambia kwamba kwa kweli tujiandae
kudanganywa. Wapo wengi watakaokuja wakitumia nafasi hii ya ujio wa Mungu ili
kutishia watu, watu waogope, watetemeke na kumbe lengo lao ni kula pesa zao tu.
Nakwambia ndugu yangu jiandae na watu kama hawa na wakija wapinge kisawa sawa.
Kingine
ni kwamba kwa kweli kitendo cha kufanya suala la ufalme wa mbinguni liwe hivi
limemfanya binadamu ajione kwamba kwa kweli yeye mwenyewe ni kiumbe dhaifu na
hivyo yafaa azidi kuwa mpole kila wakati kwani hujui siku wala saa. Hivyo
unapoishi duniani, ishi kipole, ishi vizuri na watu, usionyeshe aina yoyote ya
ubabe. Tii hekima na sheria ya Mungu. Hii ni muhimu sana.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment