MASOMO
YA MISA NOVEMBA 10, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
Hek.
6:1-11
Enyi
wafalme, sikilizeni; enyi waamuzi wa miisho ya dunia jifunzeni; sikieni ninyi
mtawalao watu wengi, na kujisifia umati wa mataifa. Kwa maana mlipewa falme
zenu na Bwana, na milki zenu na Aliye juu, ambaye atazichunguza kazi zenu, na
kuyahojihoji mashauri yenu.
Kwa
sababu, kisha kuwa wakuu wa ufalme wake, hamhukumu kwa adili, wala kuishika
torati, wala kulifuata shauri la Mungu. Yeye atawajia ghafula kwa kitisho,
madhali hukumu bila huruma huwaangukia wenye cheo; mradi mtu mnyonge aweza
kusamehewa katika rehema, bali wakuu watadumhushiwa hasa. Kwa kuwa Bwana,
Mfalme wa wote, hatajizuia kwa ajili ya mtu yeyote, wala hajali ukuu, kwa
sababu ndiye Yeye aliyewafanya wadogo na wakuu pia. Naye huwazingatia watu wote
pasipo upendeleo, walakini uchunguzi ulio halisi huwajilia wenye uwezo.
Kwa
hiyo, enyi wafalme, nawaambia ninyi maneno yangu, ili mjifunze hekima, msije
mkapotea njiani. Maana wale waliotunza kwa utakatifu mambo yale yaliyo
matakatifu watahesabiwa kuwa watakatifu wenyewe; nao wale waliofundishwa hayo
wataona neno la kujitetea. Basi fanyeni shauku ya maneno yangu; yatafuteni, na
kwa malezi yake mtapata adabu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
82:3-4,6-7 (K) 8
(K)
Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi.
Mfanyieni
hukumu maskini na yatima;
Mtendeeni
haki aliyeonewa na fukara;
Mwokoeni
maskini na mhitaji;
Mwopoeni
mikoni mwa wadhalimu. (K)
Mimi
nimesema, ndinyi miungu,
Na
wana wa Aliye juu, nyote pia.
Lakini
mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka
kama mmoja wa wakuu. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:34
Aleluya,
aleluya,
Unifahamishe
nami nitaishika sheria yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:11-19
Ikawa
walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa akipita katikati ya Samaria
na Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye
ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa,
uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa
walipokuwa wakienda walitakasika.
Na
mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti
kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je!
Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda
zako, Imani yako imekuokoa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment