ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatano,
Novemba 10, 2021.
Juma
la 32 la Mwaka
Hek
6: 1-11;
Zab
82: 3-4, 6-7 (K) 8;
Lk
17: 11-19.
SHUKRANI!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
katika asubuhi ya leo tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza. Hapa tunakutana
na mwandishi wa kitabu cha Hekima akiwaambia wanaoitwa kuwa wakuu kati ya watu
wamtambue Mungu kama mtoaji wa huo ukuu. Wasijione kana kwamba ni miungu, kana
kwamba wao kwa kitendo cha kufanikiwa kidogo sasa wana uwezo wa kila kitu ndani
ya hii dunia. Wasifikiri kwa kitendo chao cha kuheshimiwa na kusalimiwa na watu
na kuitwa wazee na waheshimiwa, wasijione kwamba ati wao wamechukua nafasi ya
Mungu.
Twaweza
kusema wakumbuke kwamba siku kadhaa zilizopita walikuwa tu wanavaa kaptura kama
wanafunzi wa primary, walikuwa maskini tu, hawakuwa wanakula hata chakula cha
mchana-lakini sasa wamepata kacheo na kuanza kuitwa waheshimiwa na wanaanza
kutaka kuchukua nafasi ya Mungu na kutaka na wao ati watawale na kuchukua
nafasi ya Mungu. Ni vizuri kuangalia kama unaiba sifa za Mungu.
Injili
ya leo inaendeleza maada hii kwa kutuonesha mfano wa watu waliofanya hivi. Hawa
walikuwa ni wale wakoma tisa kutoka Uyahudi waliokataa kurudi kwa Yesu kutoa
Shukrani zao. Hawa mwanzoni walikuwa watu maskini, wametengwa, hawana hata
nguo-sasa wanapopona wanaenda sasa huko mtaani wanaanza kuruka, labda wataanza
kuwatukana hata wenzao walio na ukoma, labda wataanza kuwapiga hata watu na kuanza
kuwaonea, Yaani walishindwa nakusahau ile hali yao ya zamani, ule ugonjwa wao,
ule unyonge wao na sasa wanajiona kuwa ni mabosi. Hata kwa Yesu hawafiki tena.
Hawa ndio wakoma wetu. Lakini siku chache zilizopita walikuwa ni ombaomba huko
lakini sasa Yesu kawaponya hawaonekani.
Labda
na kwako ndugu iko hivi. Wewe yawezekana miaka kadhaa hapo ulikuwa huna
chochote, nyumba huna na sasa umemwomba Mungu kakupa lakini umemsahau kwamba
ndiye aliyekupa na sasa unaonea wenzako, ukipita barabarani na gari hujali,
unatukana, majirani zako huwaoni kuwa kama kitu, nakwambia angalia vizuri ndugu
yangu. Kumbuka ulikotoka. Usitese watu na mali za Mungu. Mungu hakukupa ili
uwatese wenzako. Angalia utaweza kugeuka maskini baada ya masaa kadhaa.
Kingine
tujue kwamba kukataa kutoa shukrani ni kushindana na Mungu. Unataka kuchukua
nafasi yake, unataka uonekane kwamba mafanikio uliyoyapata ni ya kwako, kama
mtu anayefanya kukopi kazi ya mtu, anayetumia kazi ya mtu bila kusema
(kuaknowledge) na kujifanya ni yake-ndivyo hivyo ilivyo kwa asiyetoa shukrani.
Ni kushinda na Mungu na anayeshindana na Mungu ni shetani-ndio kazi yake.
Adhabu ya anayefanya kunakili kazi ya mtu bila kusema nakujifanya yake ni
kunyanganywa ile hadhi aliyokuwa amejinyakulia kwa kitendo chake cha kutumia hiyo
kazi ya mtu mwingine.
Hata
sasa tutambue kwamba kama tutakosa shukrani kwa Mungu, adhabu yake ni
kunyanganywa ile hadhi uliyokuwa nayo, hadhi ya kuwa wana wa Mungu.
Shetani
ndiye kiongozi wa kunakili kazi za Mungu. Siku zote anashindana na Mungu akitumia
kazi zake akijifanya ni zake ili yeye apate heshima kama za Mungu. Shetani
alishapata adhabu yake kutokana na hii kazi yake ya kunakili. Sasa usikubali
wewe kuwa namba mbili wa kuadhibiwa na Mungu kama shetani kutokana na kutumia
kazi zake na kujidai ni zako. Adhabu yako itafanana na ile ya Lucifer
alivyofukuzwa mbinguni. Wewe isije ikakupata hiyo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment