Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Novemba 15, 2021.
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
1
Mak 1: 10-15, 41-43, 54-57, 62-64;
Zab
118: 53, 61,134, 150, 155, 158;
Lk
18: 35-43.
FUNGUA
MACHO YA MOYO WANGU, NINATAKA KUKUONA WEWE
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Neno la Bwana katika
asubuhi ya leo linaongozwa na maneno ya mzaburi katika wimbo wa katikati-Ee
Bwana unijalie uhai nami nitazitii kanuni zako. Maneno haya siku ya leo
yanatuchimbulia chimbuko la somo letu la kwanza leo.
Hapa
tunakutana na simulizi ya mfalme aitwaye Antiochus Epiphanes aliyewaletea
madhara makubwa sana Waisraeli; alitaka kuangamiza Imani na tamaduni za
Kiisraeli na kufanya Mungu asiheshimiwe tena. Akaweka amri ati atakayekutwa
amebeba kitabu cha maandiko matakatifu auawe. Akawaambia watu wageukie kwenye
uabudu wa sanamu na kutolea uvumba masanamu na baadhi ya Wayahudi hasa wale
vijana vijana walikubaliana na hili wakaona sawa wakasema tuachane na hivi
visheria vyetu vya Kiyahudi, vinatubana sana, tunashindwa kuoana hata na watu
wa mataifa, tunashindwa kula raha kama watu wa mataifa. Hivyo, walianza
kukumbatia haya mambo ya kimataifa na kuiacha Imani yao.
Kitu
hiki kiliwauzi baadhi ya Wayahudi na hivyo kulitokea kikundi cha Wamakabayo
kilichopingana na huyu mfalme na wafuasi wake wote waliokuwa na lengo la
kuiteketeza dini ya Kiyahudi (Judaism). Hivyo, wimbo wa katikati unaakisi
dhamira ya hiki kikundi cha watu-unijalie uhai ee Bwana nami nitalisifu jina
lako.
Hii
ndio nia ya hawa Wamakabayo ambao kitabu chao tutakisikia kwa siku kadhaa
kadhaa. Hawa ni watetezi wa dini ya Kiyahudi. Wanasema unijalie uhai ee Bwana
nami nitakuonesha jinsi nitakavyolifanya jina lako lisifiwe, sitaliacha
lidhihakiwe na hawa watu.
Katika
somo la injili, tunakutana na kipofu anayelia Bwana nionee huruma-nionee huruma
Bwana nipate kuona. Huyu naye ukimchunguza utaona kwamba mawazo yake ni kwamba
nijalie nipate kuona ee Bwana halafu nitakuonesha namna jinsi ninavyokupenda,
nitawasimulia watu wote juu ya ukuu wako. Niponye tu na hapo utashuhudia
mwenyewe.
Ndugu
zangu, makundi yote mawili-Wamakabayo wa somo la kwanza na kipofu wa somo la
injili walifanikiwa kwa kile walichoomba. Hawakushindwa ndugu yangu kutokana na
kupania kwao kumtumikia Bwana.
Ndugu
zangu, hapa nasi tunajifunza kitu. Sisi tunashida mbalimbali, twende kwa Bwana,
mwambie ee Mungu niponye tu, nisaidie tu jamani, fanya kitu na watu wote
watashuhudia-watashuhudia jinsi nitakavyokutangaza, yaani wekeza kwangu ee
Bwana na nakwambia sitakuangusha, mwambie Bwana hivi ndugu yangu na nakwambia
atakusikiliza tu.
Lakini
siku zote uwe na lengo jema, sio kwa ajili ya kuwatesa wengine au kuwaonea
wengine au utembee mbele uitwe bosi, bosi bosi au uitwe mkuu mkuu-lengo lisiwe
hili. Lengo liwe ni kumfanya Mungu atukuzwe na si wewe uitwe mkuu, mkuuu,
jembee, jembee!
Kingine
ni kwamba huzunika popote uonapo jina la Mungu likidharaulika kama wale
Wayahudi tuliosikia katika somo la kwanza. Yaani ilifikia mahali ikawa kushika
hata yale maandiko yao matakatifu ikawa ni adhabu. Jina la Mungu wao likawa
linadhihakiwa lakini baadhi hawakuvumilia hili. Nawe ndugu yangu usikubali jina
la Mungu lidhihakiwe. Ukipita ukikutana hata na rozari imetupwa inakanyagwa
kanyagwa huko iokote, ukiona picha ya Yesu inakanyagwa huko iokote, ukiona
Biblia ipo kwenye sehemu chafu iokote na usafishe hilo eneo, ukiona vitambaa
vya altare ni vichafu na vimeshachakaa tayari kazana vingine vinunuliwe. Jina
la Bwana lisidhihakiwe hata kidogo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment