MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 15, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 33 LA MWAKA
SOMO
1
1Mak.
1:10-15, 41-43, 54-57, 62-64
Kulichipuka
chipukizi chenye dhambi, ndiye Antioko Epifani, mwana wa mfalme Antioko, ambaye
alikuwa amewekwa amana kwa Warumi. Naye alitawalishwa katika mwaka wa mia
thelathini na saba wa enzi ya Wayunani.
Siku
zile walitokea wahalifu sheria katika Israeli, wakashawishi wengi, wakisema,
Twende tufanye maagano na mataifa wanaotuzunguka, maana tangu tulipofarakana
nao misiba mingi imetupata. Jambo hilo likapendeza machoni pao, hata watu
Fulani wakafanya hima kwenda kwa mfalme, naye akawapa ruhusa kuzifuata kawaida
za mataifa. Wakafanya kiwanja cha michezo Yerusalemu kama kawaida ya mataifa,
wakajifanya kana kwamba hawakutahiriwa wakajitenga na agano takatifu. Hivyo
walijiunga na mataifa na kujiuza wafanye uovu.
Mfalme
Antioko akaziandikia milki zake zote, kwamba wote wawe taifa moja, kila mtu
aache sheria zake za asili. Watu wote wa mataifa wakaikubali amri ya mfalme,
hata wengi katika Israeli walifuata ibada yake, wakitoa dhabihu kwa miungu ya
uongo na kutia unajisi Sabato.
Siku
ya ishirini na tano ya Kislevu, mwaka wa mia arobaini na tano, waliweka chukizo
la uharibifu juu ya madhabahu, na katika miji ya Uyahudi kila upande walijenga
vimadhabahu vya miungu, wakavukiza uvumba milangoni pa nyumba na njiani. Na
vitabu vya sheria walivyovipata waliviparua vipande vipande wakaviteketeza. Mtu
yeyote aliyepatikana na kitabu, au aliyeonekana anaifuata sheria, alihukumiwa
kufa kama alivyoamuru mfalme.
Hata
hivyo wengi katika Israeli walikaza nia zao kwa uthabiti wasile vitu vilivyo
najisi. Waliona afadhali kufa kuliko kutiwa unajisi kwa vyakula au kulivunja
agano takatifu. Wakafa. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
119:53, 61, 134, 150, 155, 158 (K) 88
(K)
Unihuishe kwa fadhili zako, nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
Ghadhabu
imenishika kwa sababu ya wasio haki,
Waiachao
sheria yako.
Kamba
za wasio haki zimenifunga,
Sikuisahau
sheria yako. (K)
Unikomboe
na dhuluma ya mwanadamu,
Nipate
kuyashika mausia yako.
Wanakaribia
wanaonifuatia kwa chuki,
Wamekwenda
mbali na sheria yako. (K)
Wokovu
u mbali na wasio haki,
Kwa
maana hawajifunzi amri zako.
Nimewaona
watendao uhaini nikachukizwa,
Kwa
sababu hawakulitii neno lako. (K)
SHANGILIO
Zab.
147:12, 15
Aleluya,
aleluya,
Msifu
Bwana, Ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
INJILI
Lk.
18:35-43
Yesu
alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba
sadaka; na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini? Wakamwambia,
Yesu wa Nazareti anapita. Akapiga kelele, akisema, Yesu Mwana wa Daudi,
unirehemu. Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi
sana kupaza sauti, Ee mwana wa Daudi, unirehemu.
Yesu
akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza, Wataka
nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona. Yesu akamwambia, Upewe kuona;
imani yako imekuponya. Mara hiyo akapata kuona. Akamfuata, huku akimtukuza
Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment