MASOMO YA MISA, JUNI 10,
2021
ALHAMISI, JUMA LA 10 LA
MWAKA
SOMO 1
2Kor. 3:15-4:1, 3-6
Hata leo, torati ya Musa
isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana,
ule utaji huondolewa. Basi ‘Bwana’ ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana,
hapo ndipo penye uhuru. Lakni sisi oste, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha
utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo
huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye
Roho.
Kwa sababu hiyo, kwa kuwa
tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei. Lakini ikiwa injili
yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa
dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya
utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali
Kristu Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili
ya Yesu. Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa
mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu
Kristo.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 85:8-13 (K) 9
(K) Utukufu wake ukae
katika nchi yetu.
Nisikie atakavyosema
Mungu Bwana,
Maana atawaambia watu
wake amani,
Naam, na watauwa wake
pia,
Bali wasiurudie upumbavu
tena.
Hakika wokovu wake u
karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi
yetu. (K)
Fadhili na kweli
zimekutana,
Haki na amani
zimebusiana.
Kweli imechipuka katika
nchi,
Haki imechungulia kutoka
mbinguni. (K)
Naam, Bwana atatoa
kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao
yake.
Haki itakwenda mbele
zake,
Nayo itazifanya hatua
zake kuwa njia. (K)
SHANGILIO
Efe. 1:17,18
Aleluya, aleluya.
Mungu wa Bwana wetu Yesu
Kristu, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
INJILI
Mt. 5:20-26
Yesu aliwaambia wanafunzi
wake: Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia
kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mmesikia watu wa kale
walivyoambiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni,
Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake,
itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta
sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu
yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu
yako, kasha urudi uitoe sadaka yako. Patina na mshitaki wako upesi, wakati
uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi
akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe
hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment