MASOMO YA MISA, Mei 25,
2021
JUMANNE, JUMA LA 8 LA
MWAKA
SOMO 1
YbS. 35 : 1-12
Mwenye kuishika torati
ndiye azidishaye matoleo; mwenye kuziangalia amri ndiye aitoaye kafara ya
amani; amlipaye mwenzake hisani yake hutoa sadaka ya unga bora; naye atoaye
sadaka kwake maskini hutoa dhabihu ya kushukuru. Kuuacha uovu kwampendeza
Bwana, na kujitenga na udhalimu ni kipatanisho. Lakini ujihadhari usitokee
mbele za Bwana mikono mitupu; maana sharti hayo yote yatendeke kwa ajili ya amri.
Toleo lake mwenye haki lina kibali madhabahuni, na harufu tamu yake yafika
mbele zake Aliye juu. Dhabihu ya mwenye haki yakubalikana, wala kumbukumbu lake
halisahauliki.
Umheshimu Bwana kwa jicho
la ukarimu, wala usimtolee malimbuko ya kazi za mikono yako kwra ubahili. Kwa
kila kitolewacho uonyeshe ukunjufu wa uso, hata sehemu ya kumi uiweke wakfu kwa
changamko. Mpe Mungu kama alivyokupa wewe; na kama mkono wako ulivyopata, utoe
kwa ukarimu. Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye ni nani awezaye kulipa
isipokuwa ni yeye; kwa kuwa Bwana hulipa, naye atakulipa wewe mara saba.
Usidhanie kuwa unaweza
kutoa rushwa, kwa maana Yeye hazipokei; wala usiwaze moyoni kutoa dhabihu ya
jeuri, kwa kuwa Bwana ndiya mhukumu wala hakijali cheo cha mtu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 50 : 5-8, 14, 23 (K)
23
(K) Nitamwonyesha wokovu
wa Mungu autengenezaye mwenendo wake.
Nikusanyieni wacha Mungu
wangu
Waliofanya agano nami kwa
dhabihu.
Na mbingu zitatangaza
haki yake,
Kwa maana Mungu ndiye
aliye hakimu.
Sikieni, enyi watu wangu,
nami nitanena,
Mimi nitakushuhudia,
Israeli;
Mimi ndimi niliye Mungu,
Mungu wako.
Sitakukemea kwa ajili ya
dhabihu zako,
Na kafara zako ziko mbele
zangu daima. (K)
Mtolee Mungu dhabihu za
kushukuru,
Mtimizie Aliye iuu
nadhiri zako.
Atoaye dhabihu za
kushukuru,
Ndiye anayenitukuza.
Naye autengenezaye
mwenendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wa
Mungu. (K)
SHANGILIO
LK 8:15
Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno la
Mungu. Aleluya.
INJILI
Mk. 10:28-31
Petro alimwambia Yesu,
Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akasema, Amin, nawaambieni,
Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba,
au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa
mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na. mama, na
watoto na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa
kwanza.
Neno la Bwana... Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment