“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Mei 25, 2021
Juma la 8 la mwaka wa
Kanisa
YbS 35: 1-12;
Zab 50: 5-8;
Mk 10: 28-31.
KUMFUATA YESU BILA
MASHARTI!
Karibuni ndugu zangu
wapendwa kwa tafakari ya neno la Mungu katika adhimisho la Misa Takatifu. Leo
miongoni mwa ujumbe tunaopewa na Yoshua bin Sira ni kufanya urafiki na Mungu
kwa mali ya dunia tuliyonayo. Chochote ulichopewa na Mungu-hata kama ni uwezo
wako wa kiakili, ujuzi mzuri, fedha, uwezo wa kueleza na kufafanua mambo,
lazima tuutumie kuanzisha nao urafiki na Bwana. Tuwe wakarimu katika kuanzisha
urafiki huu, hata kama ni cheo chako na madaraka yatumie vizuri wakati huu
kuanzisha urafiki na Bwana.
Tumia ujuzi wako, kazi
yako ofisini, tuwe tayari kuanzisha urafiki huu na hakika tutafanikiwa mnoo.
Usikubali nyumba ya Mungu ibaki mahame wakati wewe unakaa sehemu za kungaa na
za hali ya juu, toa michango na kujitoa kuhakikisha sehemu ya Mungu ni nzuri,
usikubali nyumba ya rafiki yako ( Yesu alituita rafiki) iwe mahame, itunze na
lijali kanisa zaidi na zaidi. Tutafanikiwa sana.
Lakini wengi wetu-kadiri
tunapopata mali urafiki wetu na Mungu unapotea polepole, tunapatwa na kiwewe
cha kutenda uovu na kutufanya tukosane na Mwenyezi Mungu. Wapo wanaotumia
umaarufu wao au uzuri wao au fedha zao kutenda uovu. Hii ni sababu ya wengi
kunyanganywa nafasi walizopewa na Bwana. Tutambue uchoyo kwa Mwenyezu Mungu
ndicho chanzo, mwanzo wa wengi wetu kuanguka. Tujitahidi kuondokana na uchoyo
mbele ya Mungu.
Katika somo la Injili
Yesu anadhihirisha kwamba aliyemkarimu kwa Bwana hupokea zaidi. Anawaeleza
wanafunzi wake kwamba kama watakuwa tayari kujitoa kwa Bwana, hakika watapokea
mara mia, sisi tuzidi kuwa wakarimu kwa Bwana. Wengi wamebarikiwa kwa ukarimu
kwa Bwana. Wapo wachoyo wanaoficha vitu lakini hawaendelei, kila siku wanarudi
nyuma licha ya kuficha na kujikusanyia. Tuwe tayari kutoa muda wetu kwa sala,
kusaidia maskini, na kufanya shughuli zetu, hapa ndipo tutakapo barikiwa. Tuwe
wakarimu wa kutumia nguvu zetu, vipaji vyetu na vyeo vyetu kumtangaza Bwana.
Tuache uchoyo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment