MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 9, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 5 LA MWAKA
SOMO
1
Mwa.
1:20 – 2:4
Mungu
alisema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege
waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na
kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kw
ajinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni
vyema. Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya
baharini, ndege na wazidi katika nchi. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
Mungu
akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufungwa, nacho
kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya
mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufungwa kwa jinsi zake, na kila
kitu kitaambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mungu
akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu; kwa sura yetu; wakatawale samaki wa
baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano
wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mungu
akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na
kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche
utoao mbegu, ulio juu ya uso wan chi yote, pia, na kila mti, ambao matunda yake
yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wan chi,
na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye
uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila
kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku
ya sita.
Basi
mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu
alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya
kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa
sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote
aliyoiumba na kuifanya.
Hivyo
ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
8:3 – 8 (K) 1
(K)
Wewe Mungu, Bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote.
Nikiziangalia
mbingu zako, kazi ya vidole vyako,
Mwezi
na nyota ulizoziratibisha;
Mtu
ni kitu gani hata umkumbuke,
Na
binadamu hata umwangalie? (K)
Umemfanya
mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika
taji ya utukufu na heshima;
Umemtawaza
juu ya kazi ya mikono yako;
Umevitia
vitu vyote chini ya miguu yake. (K)
Kondoo,
na ng’ombe wote pia;
Naam,
na wanyama wa kondeni;
Ndege
wa angani, na samaki wa baharini;
Na
kila kipitiacho njia za baharini. (K)
SHANGILIO
Zab.
27:11
Aleluya,
aleluya,
Ee
Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
INJILI
Mk.
7:1-13
Mafarisayo,
na badhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele ya Yesu,
wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani,
isiyonawiwa. Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka
kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; tena wakitoka sokoni,
wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha
vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.
Basi
wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata
mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? Akawambia, Isaya
alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa
huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami; Nao waniabudu bure,
wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.
Ninyi
mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Akawaambia, Vema?
Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. Maana Musa alisema,
Waheshimu baba yako na mama yako, na, amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. Bali
ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye. Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu
changu chochote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; wala hammruhusu baada
ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; huku mkilitangua neno la Mungu kwa
mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment