MASOMO YA MISA, FEBRUARI 22, 2021,
JUMA LA 6 LA MWAKA WA KANISA
SIKUKUU
YA UKULU WA MT. PETRO (MTUME)
SOMO
1
1Pet.
5:1 – 4
Nawasihi
wazee walio kwenu, mimi niliye mzee mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo,
na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; lichungeni kundi la Mungu lililo
kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo;
si kkwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana
juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji
mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
23 (K) 1
(K)
Bwana ndiye mchungaji wangu
Bwana
ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa
na kitu.
Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando
ya maji ya utulivu huniongoza. (K)
Huniuisha
nafsi yangu, na kuniongoza,
Katika
njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam
nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa
mabaya,
Kwa
maana wewe upo pamoja nami,
Gongo
lako na fimbo yako vyanifariji. (K)
Waandaa
meza mbele yangu,
Machoni
pa watesi wangu.
Umenipaka
mafuta kichwani pangu,
Na
kikombe changu kinafurika. (K)
Hakika
wema na fadhili zitanifuata,
Siku
zote za maisha yangu,
Nami
nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SHANGILIO
Mt.
16:18
Aleluya,
aleluya,
Wewe
ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya
kuzimu haitalishinda.
Aleluya.
INJILI
Mt.
16:13 – 19
Yesu
alienda pande za Kaisaria – Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu
hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohane
Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia,
Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiye
Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni
Baryona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye
mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga
kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo
za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa
mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment