“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Februari 27, 2021,
Juma
la 1 la Kwaresima
Kumb
26: 16-19;
Zab
119: 1-2, 4-5, 7-8;
Mt
5: 43-48
KUTAMANI
KUWA MKAMILIFU
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la misa asubuhi ya leo. Leo tafakari ya neno la Bwana
tutaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa katikati hapa tunakutana na
zaburi inayosema kwamba heri walio kamili katika njia za Bwana; heri wale
waishikao sheria ya Bwana kwani Bwana atawabariki daima na kuwa mfano kwa
wengine; watu wakiwaona watatiwa matumaini. Haya ni maneno ya mzaburi wetu.
Maneno haya yanaambatana vyema na maneno ya ujumbe wa neno la Bwana katika somo
la kwanza ambapo Musa anawaambia wana wa Israleli wawe waaminifu kwa zile
sheria za Mungu walizomwahidia kuzishika. Kwa kuzishika sheria hizi, Mwenyezi
Mungu anaahidi kuwabariki na kuwafanya kuwa taifa kubwa sana. Nao watalifanya
jina lake liheshimiwe pote na watu wote watakuja kwa Mungu wa Israeli kumwabudu
na hivyo Mungu wa Israeli atapata sifa. Hii ndiyo faida ya kuzishika amiri za
Mungu.
Ndugu
yangu, jua kwamba unapoishika amri ya Mungu, unamfanya Mungu asifike, apate
sifa na utukufu. Mfano, kitendo cha mashahidi kufa kwa ajili ya Yesu,
kilimfanya Yesu atukuke, apate utukufu. Hivyo, ndugu zangu, tujitahidi leo.
Tuzishike amri za Mungu, tukizishika tunawafanya wenzetu wamsifu na kumtukuza
Mungu. Unapokataa kuzishika amri unawakwaza wenzako na Mungu atatukanwa kila
kukicha ndugu zangu. Siku hizi Yesu anadharauliwa na baadhi ya watu Fulani kwa
sababu tumeshindwa kuonyesha mfano mzuri na watu kuishia kumdharau Yesu.
Injili
yetu inatuambia kwamba lazima sisi kama Wakristo maisha yetu yaonyeshe
utofauti. Nisi ishi kwa kuongozwa na mitazamo ya watu wa dunia. Wanadamu wengi
tunafuata siasa ya jino kwa jino, ninakulipa kile ninachopokea kutoka kwako.
Ninakuwa rafiki kwa yule ninayejua kwamba naye ni rafiki, namsaidia yule
nijuaye kwamba atakuja kunisaidia baadaye. Yesu anapinga hili na kusema kwamba
tunapofanya hivi ni kinyume cha wito wetu, hufanyi cha ziada kwani hata wenye
dhambi hujifanyia hivi hivi-hivyo tukifanya hivi hatutakuwa tofauti na wenye
dhambi. Sisi tunategemewa kufanya Zaidi-na anayeshika dini anategemewa afanye
Zaidi. Mfano, kosa moja laweza kufanywa na watu wawli tofauti-lakini unashangaa
watu wanauliza limefanywa na nani. Unapokutwa limefanywa na mkristo au mtu wa
dini, basi malalamiko yanakuwa makubwa Zaidi. Hivyo, tujue kwamba tunategemewa
kutenda Zaidi kama watu wa dini. Fundisho hili litupe nguvu na moyo wa
kuwasaidia maskini na wenye shida tunaokutana nao kila siku. Hawa hawawezi
kutulipa na kama hatutaelewa fundisho hili la Yesu, kamwe hatutaweza
kuwasaidia. Wakituomba mchango hatutawapa. Lakini kama tutaelewa fundisho la
Yesu, basi tutakuwa radhi kuwaasaidia muda wote. Fundisho hili litutie moyo
katika kujitolea Zaidi kwa ajili ya maskini. Tumsifu yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment