MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 17, 2021
KIPINDI
CHA KWARESIMA
JUMATANO
YA MAJIVU
SOMO
1
Yoe.
2:12-18
Lakini
hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa
kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie
Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi
wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. N’nani ajuaye kwamba
hatarudi na kugeuka, na kutuachia Baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na
sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?
Pigeni
tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; kusanyeni
watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, na hao wanyonyao
maziwa; bwana arusi na toke chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.
Hao
makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu, na
waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, wala usiutoe urithi wako upate aibu,
hata mataifa watawale juu yao; kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Hapo
ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
51:1-4, 10-12, 15 (K) 1
(K)
Uturehemu, Ee Bwana, kwa kuwa tumetenda dhambi.
Ee
Mungu, nirehemu,
Sawasawa
na fadhili zako.
Kiasi
cha wingi wa rehema zako,
Uyafute
makosa yangu.
Unioshe
kabisa na uovu wangu,
Unitakase
dhambi zangu. (K)
Maana
nimejua mimi makosa yangu,
Na
dhambi yangu I mbele yangu daima.
Nimekutenda
dhambi Wewe peke yako,
Na
kufanya maovu mbele za macho yako. (K)
Ee
Mungu, uniumbie moyo safi,
Uifanye
upya roho iliyotulia ndani yangu
Usinitenge
na uso wako,
Wala
roho yako mtakatifu usiniondolee. (K)
Unirudishie
furaha ya wokovu wako;
Unitegemeze
kwa roho ya wepesi.
Ee
Bwana, uifumbue midomo yangu,
Na
kinywa change kitazinena sifa zako. (K)
SOMO
2
2
Kor. 5:20 – 6:2
Ndugu
zangu, basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa
vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Yeye
asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki
ya Mungu katika Yeye.
Nasi
tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. Kwa maana
asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nilikusaidia; tazama,
wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Zab.
95:8
Msifanye
migumu mioyo yenu; msikie sauti ya Bwana.
INJILI
Mt.
6:1-6, 16-18
Angalieni
msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya
kama hayo, hampatai thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo
sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na
njiani, ili watukuzwe na watu. Amini, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu
yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono
wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Tena
msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama
katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amini,
nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika
chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako
aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Tena
mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso
zao, ili waonekane na watu kuwa nafunga, Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata
thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili
usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako
aonaye sirini atakujazi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment