“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kwaresima
Jumatano,
Februari 17, 2021
Jumatano
ya majivu (Siku ya kufunga na kujinyima)
Yoel
2: 2-18;
Zab
51: 3-17;
2
Kor 5:20 – 6:2
Mt
6: 1-6, 16-18
KUTOKA
MAJIVU MPAKA KWENYE UTUKUFU!
Leo
tumeanza kipindi cha neema cha Kwaresima, na tunaitwa kusali, kutolea sadaka na
matendo ya huruma. Tukiwa tunatafakari kipindi hichi, tukiangalia mbele katika
kuadhimisha mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo. Maisha ya toba
na kuongoka ndio maada kuu ya Kwaresima.
Katika
somo la kwanza ujumbe wa wongovu umetengenezwa na maneno haya “mrudieni Mungu
kwa mioyo yenu yote” (Yoel 2:12). Kwa Yoeli, kuongoka ni njia ya kurudi nyuma.
Wale wote waliojiweka katika njia isio sawa wanaitwa kurudi nyuma. Katika somo
la pili Paulo anaongelea kuhusu upatanisho. Anasema “tunaomba Mungu
awapatanishe” upatanisho na Mungu unapatikana kwa kuishi ujumbe unaoletwa kwetu
na wajumbe wa Mungu-wajumbe waneno lake (Warumi 10:14, 17).
Katika
somo la Injili Yesu anaongelea mara saba tuzo ambalo wanalipokea wale
wanaotenda kadiri ya mafundisho yake. Injili mara nyingi inaelezea kuhusu
‘tuzo’ walilowekewa wenye haki na ‘adhabu’ kwa walio waovu. Tuzo analo
liongelea Yesu, sio kuwa na sehemu nzuri ya juu mbinguni bali , kuongezeka
mapendo, hali ya muunganiko wa ndani, na hali ya kufanana na uso wa Baba wa
mbinguni. ‘Tuzo’ ni furaha ya upendo wa hali ya juu, kama Mungu anavyofanya, ni
hali ya “kuwepo katika ufalme wake”. Kukuwa katika hali hii ya juu, katika
mwanzo wa kwaresima Yesu anatualika tufanye mambo matatu: kutolea sadaka, sala
na kufunga. Hizi zinajenga nguzo tatu za kiroho za Wayahudi, na yeye anaziweka
tena lakini katika hali yake ya kipekee.
Sadaka:
katika kipindi cha Yesu, baadhi ya watu walikuwa wana jukumu la kukusanya na
kugawa sadaka kwa maskini, yatima, wajane na wasio jiweza. Wakati wa Sabato,
kulikuwa na tabia ya kuwasifia wale waliotoa nyingi na walitangazwa mbele ya
mikusanyiko. Kwa Yesu, kutoa sadaka sio kuweka hela kidogo, bali kuwa na haki,
ni kutambua kuwa vitu vyote vya dunia sio vyetu ni vya Mungu. Kil aliyechukuwa
zaidi anapaswa kurudisha kwa wale wasio nacho. Mt. Ambrose, aliwaambia matajiri
“kumbuka kwamba, hamuwapi maskini kilicho chenu; bali mnawapa tu kile kilicho
mali yao”
Sala:
wakati wa kipindi cha Yesu kulikuwa na aina mbili za sala: sala ya pamoja na
sala binafsi. Sala za pamoja, zilifanywa hekaluni, katika masinagogi na katika
mitaa, mara mbili kwa siku. Yesu hakatazi matendo haya. Yeye anaelekeza macho
yake zaidi kwenye sala ya binafsi, ambayo inafanywa na mtu mwenyewe, milango
imefungwa katika hali ya muunganiko wa ndani na Baba “anaye ona vyote”. Sala
hii sio marudio ya fomula mbali mbali, bali ni mazungumzo na Mungu, nikumwomba
asikilize mapenzi yetu na kutimiza ndoto zetu, lakini pia kuishi mapenzi yake
na kupokea kutoka kwake majukumu aliotupangia ya kujenga ufalme wake. Sala,
kwanza kabla ya yote ni kusikiliza, kufungua mioyo yetu na kukaribisha mipango
ya Mungu na bila kukiuka matazamio yake.
Kufunga:
katika kipindi cha Yesu, waliamini kwamba kufunga kwa kweli ilileta baraka
kubwa sana: ilisaidia kuacha dhambi, na kumfanya Bwana aone huruma, kuepuka
adhabu yake, na kukinga na mabaya yote. Kufunga kwa Mkristo haihitaji
kutambulika. Wanaosha nyuso zao na kuonekana wenye furaha, ana furaha kwasababu
kwa kujinyima kwake anamuona maskini akifurahia kutumia ulichompa. Kufunga
kuliko kubalika na Mungu ni “kuvunja aina zote za ukosefu wa haki….funga kwa
kushirikisha mkate wako na wale walio na njaa, walete katika nyumba yako wasio
na nyumbani, wavalishe wale walio uchi” (Isa 58:6-7). “kuweni wakarimu kati
yenu …msiweke maovu juu ya mwingine ndani ya moyo yenu” (Zek 7:5-10).
Katika
mwanzo wa kwaresima tunakumbushwa kwamba Kwaresima inaanza na majivu na kuishia
na moto, moto wa pasaka wa ufufuko na moto wa Roho Mtakatifu wakati wa
Pentekoste, uhakika wa jinsi tutakavyo kuwa. Yesu amezamisha uwepo wetu ambao
ni vumbi na majivu katika damu yake, na kutuwezesha kufufuka katika maisha
mapya. Roho Mtakatifu anatufanya viumbe vipya.
Sala:
Bwana, ninaomba kwaresima hii iwe yenye matunda katika maisha yangu. Ninaomba
kiwe kipindi cha neema cha kukumbatia yote unayotaka niyafanye ndani yangu.
Yesu, nakuamini wewe. Amina
Tabia
takatifu ya Kwaresima: SALA- Bwana nisaidie mimi nijifunze tabia ya kusali, ya
kuwa karibu nawe. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment