Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

NJIA YA MSALABA JUU YA HURUMA YA MUNGU

 NJIA YA MSALABA JUU YA HURUMA YA MUNGU


(Unaweza ukaongeza sala zako binafisi mfano,Baba yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba na wimbo wowote  katikati kwa kila kituo cha njia ya msalaba. Nukuu kutoka BIBLIA na ‘Huruma ya Mungu katika Roho Yangu: Diary ya Mtakatifu Maria Faustina Kowalska’ )


Kabla ya kila kituo: 

K: Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru;

W: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.


Baada ya kila kituo:

'Baba Yetu-, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe',

K: Ee Bwana utuhurumie! W: Utuhurumie!

K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina



SALA YA MWANZO:

Baba mwenye huruma, bwana wangu, nataka kukufuata kwa imani. Nataka nikuige we we katika maisha yangu katika hali kamilifu kabisa. Ndiyo maana naomba katika tafakari yangu ya njia ya msalaba, utanikirimu neema ya uelrea mkubwa wa maajabu yapatikanayo katika maisha ya kiroho. Bikira Maria mama Wa Huruma, Siku zote mwaminifu kwa Kristo Yesu, niongoze katika njia ya mateso na niombee Baraka tele katika kutafakari njia hii ya msalaba.




1. KITUO CHA KWANZA - YESU ANAHUKUMIWA AFE.

Somo:  Mk 26: 59-60 


Yesu kwa Mt. Faustina: Yesu kwa Mt. Faustina : Usishangae kwamba Mara nyingine unapata tuhuma mbaya tens za uongo za kusingiziwa. Mm mwenyewe nimekunywa kikombe cha mateso haya kwa ajili ya upendo wangu kwako(289). Nilipokuwa mbele ya Herode, nilipata neema kwa ajili yako, kwamba utaweza vumilia mateso yote ya hapa duniani na utafuata njia yangu.(1164). 


Mt. Faustina: Tupo making sana kwa maneno tuambiwayo, na tunataka kujibu haraka,bila kujali ni mpango Wa Mungu lazima uongee. Moyo mkimya una nguvu sana, hakuna kitakacho dhuru moyo mkimya kama ukiweza kuvumilia. Moyo uliokatika hali ya ukimya unaweza ukawa na muungano Wa karibu sana na Mungu. (477). 


Sala: Yesu mwenye huruma, nisaidie kutambua jinsi ya kukubali mafikirio ya kibinadamu hasa ya kumtuhumu binadamu mwenzio kwa jambo Fulani ambalo silo la kweli.



2. KITUO CHA PILI - YESU ANAPOKEA MSALABA.

Somo: Yn 19:1-6


Yesu kwa Mt. Faustina: Usiogope mateso, nipo pamoja nawe(151). Jinsi utakavyopenda mateso, ndivyo utakavyo kuwa na upendo thabiti kwangu. (279)


Mt. Faustina:  Yesu nakushukuru kwa misalaba midogodogo, kwa kupingwa kwa mawazo yangu na jitihada zangu, kwa ugumu Wa maisha ya jumuiya, kwa kupata pingamizi toka kwa binadamu wenzangu kwa mawazo yangu,kwa kupata  manyanyaso toka kwa binadamu wengine, kwa kudhaniwa vibaya, kwa Huduma mbaya ya afya na kupoteza nguvu, kwa kujikana nafsi yangu mwenyewe, na kwa kujiua mwenyewe, kwa kukosa kujitambua mwenyewe kwa kukata tamaa kwa mawazo na mipango yangu. (343).


Sala: Yesu mwenye huruma , nifundishe jinsi ya kuthamini ugumu  maisha yangu, makwazo na mateso ninayopitia. Nisaidie nibebe misalaba hii kwa upendo thabiti.



3. KITUO CHA TATU - YESU ANAANGUKA MARA YA KWANZA.

Somo Isa 53:6,12. 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Maovu  tunayofanya kwa kukusudia hayawezi nizuia kuonesha upendo wangu ila maovu yanayofanywa kwa makusudi upendo na rehema yangu haiwezi onekana kwa watu hawa. (1641). 


Mt. Faustina:  Yesu wangu mbali na neema zote unazonijalia bado naona maovu na madhambi yangu kwako kuwa yanakuumiza. Mungu nisaidie nisikate tamaaa niendelee kukupenda wewe kwani upendo wako na rehema zako kwangu in thabiti Bwana Wa Majeshi (606). 


Sala: Bwana Wa huruma, nilinde kwani nimekutenda dhambi nihurumie.



4. KITUO CHA NNE - YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKA

Somo: Lk 2:34-35 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Yesu anakutana na mama yake. Yesu. Japo kazi zote nizifanyazo napitia mateso makali mno, nachukulia kama haya yanayoonekana hayajapata mateso kama kazi ambazo ni moja kwa moja zangu hasa kazi ya ukombozi.  (1643). 


Mt. Faustina:  Nilimwona Bikira Maria akiwa katika uzuri Wa ajabu. Alinishika karibu yake na kuniambia, Mimi ni mama yenu nyote na tumshukuru kwa huruma yake kwetu sisi wanadamu. Kinachonitia moyo zaidi Mimi ni kwamba kuna zile roho ambazo zinafanya matendo ya Mungu. Kuwa na ujasiri. Usiogope makwazo upatayo lakini weka matumaini yote kwake akutiaye nguvu. (449). 


Sala: Maria mama Wa Mungu mama Wa huruma, kuwa karibu nami hasa katika mateso kama ulivyo kuwa kwa mwanao katika mateso msalabani.



5. KITUO CHA TANO - SIMONI WA KIRENE ANABEBESHWA MSALABA AUCHUKUE NYUMA YA YESU

Somo: Lk 23:26 


Yesu kwa Mt. Faustina: Usiku na mchana namjalia Baraka kwa kijana huyu. Nawahimiza mwige mfano wake. Sizawadii mtu kwa matokeo mazuri ila kwa jitihada na moyo aliokuwa nayo, moyo wa upendo na dhati katika kutimiza jambo hill..hata kama halikufanikiwa ilimradi lilifanywa kulingana na matakwa yangu. (86). 


Mt. Faustina:  Yesu hutoi zawadi kwa wale waliofanikiwa tu, Bali kwa wale waliokuwa wanafanya kwa moyo Wa upendo na uvumilivu kwa ajili yangu. Hivyo basi nimepata faraja kwani hata kama nisipofanikiwa kwa yale  inayofanya kwa ajili take, bado yupo na Mimi (952). 


Sala: Bwana Yesu naomba nijalie mawazo, maneno na matendo yangu nifanye kwa upendo wako. Bariki nia zangu zote Baba.



6. KITUO CHA SITA - VERONIKA ANAUPANGUSA USO WA YESU

Somo: Isa 53:2-3 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Tambueni kwamba chochote kizuri mnachokifanya kwa yoyote yule, nakipokea kama vile mmenifanyia Mimi. (1768). 


Mt. Faustina:  Najifunza jinsi ya kuwa mwema kupitia kwa Yesu, ambaye ndiye WEMA, ili niweze kuitwa mwana Wa Baba Wa Mbinguni (669). Upendo mkubwa huweza kubadikisha vitu vidogo kuwa vitu vikubwa, na ni upendo tu ndio unayapa thamani matendo yetu (303). 


Sala: Bwana Yesu na Bwana wangu, bariki macho yangu, mikono yangu, midomo yangu na moyo wangu siku zote viwe na huruma. Nibadilishe niwe mtu wa huruma.



7. KITUO CHA SABA - YESU ANAANGUKA MARA YA PILI

Somo: Isa 53:4 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Chanzo cha maanguko yenu ni kwasababu mmejiamini sana wenyewe bila kuweka matumaini yenu kwangu. But jambo hili lisiwakatishe tamaa sana. Tambueni kwamba Mungu wenu ni Mungu wa huruma (1488). Tambueni pia kuwa kwa ninyi wenyewe tu, hamuwezi kitu bila Mimi (639). Bila msaada toka kwangu hamuezi kupata Baraka zangu (738). 


Mt. Faustina:  Yesu, usiniache mwenyewe katika mateso. Nafahamu unatambua udhaifu wangu ulivyo. Mimi sio chochote mbele yako, nini kitakuwa kipya kwako kama ukiniacha nianguke mwenyewe? (1489). Yesu, simama kwangu Baba kama mama kwa mtoto asiye na msaada wowote ule. (264). 


Sala: Mungu naomba rehema zako zinisaidie, ili nisiwe naanguka Mara kwa Mara, na nikianguka nisaidie kuinuka tena.



8. KITUO CHA NANE - AKINA MAMA WANAMLILIA YESU

Somo: Lk 23:27-28 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Jinsi ninavyovutiwa kwa nwenye Imani.! (1420). Waambieni wote kwamba natamani niwaone wakiishi roho ya Imani. (353). 


Mt. Faustina: Namuomba Bwana Yesu aimarishe Imani yangu, ili niweze kuvumilia yote katika maisha yangu, nisijisahau na kuongozwa na matendo ya wanadamu Bali niongozwe na matendo ya wanadamu wanayo Fanya kwa moyo Wa upendo na wanaongozwa na roho ya Bwana. Ni ajabu jinsi kila kitu hapa duniani kinavyo muongoza mwanadamu! Lakini kuishi kwa imani kutazidi kutufanya tuweze kuitwa watoto Wa Mungu na kutuwezesha kufanya mambo yetu kwa upendo zaidi. (210). 


Sala: Bwana mwenye huruma, nakushukuru kwa ubatizo, na rehema ya imani. Kila Mara nakuita Ee Yesu, nakutumainia, ongeza imani yangu..



9.  KITUO CHA TISA - YESU ANAANGUKA MARA YA TATU

Somo: Isa 53:7-10 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Mwanangu, tambua kuwa kikwazo kikubwa kuelekea utakatifu, ni kukubali na kukatishwa tamaa na makwazo. Haya yatakufanya hata ushindwe kutenda mema. Usikate tamaa katika kurudi kuomba msamaha, kwani nipo tayari siku zote kukusamehe. Kama ukiomba msamaha, basi unatukuza huruma yangu. (1488) 


Mt. Faustina:  My Jesus, despite your graces, I see and feel all my misery. I begin my day with battle and end it with Yesu wangu, mbali na rehema zako, bado naona udhaifu wangu. Naanza siku yangu kwa mapambano na maliza kwa mapambano. Ninapomaliza kupigana na kikwazo kimoja, vingine kumi vinakuja tena. Ila sins wasiwasi hata kidogo, kwani natambua hiki ni kipindi cha mapambano sio Amani. (606). 


Sala:  Bwana mwenye huruma, najiachia kwako, nikiwa na mapungufu ya kibinadamu. Nakuomba madhaifu yangu yaondolewe kwa upendo na huruma yako.



10. KITUO CHA KUMI - YESU ANAVULIWA NGUO

Somo: Jn 19:23-24


Mt. Faustina:  Yesu alisimama mbele yangu, kavuliwa Nguo na mwili wake umejaa vidonda, macho yake yamejaa machozi na damu na uso wake umeharibika kabisa hautamaniki.


Yesu kwa Mt. Faustina:  Mwanamwali hana budi kufanana na mchumba wake.


Mt. Faustina:  Naelewa maneno haya kwa undani wake. Hakuna sehemu ya kuwa na wasiwasi hapa. Kufanana kwangu na Yesu lazima niwe mtu Wa mateso pia na huruma.humility (268). 


Sala: Ee Yesu, mwingi wa huruma na upendo, naomba fanya moyo wangu kama wako.



11. KITUO CHA KUMI NA MOJA - YESU ANASULUBISHWA MSALABANI

Somo: Mt 27:39-43 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Wanangu, kuweni na upendo kwa wale wan sodas a babushka mateso. Watetendeni mema wale wanaowachukia. (1628). 


Mt. Faustina:  Ee Yesu wangu, unatambua nguvu gani zinahitajika kuishi na wale ambao mioyo yetu haiwapendi yaani wale maadui wetu wanaotusababishia mateso. Kibinadamu, hii sio rahisi. Kwa kipindi hiki najaribu kumtambua Yesu katika mtu huyo anaenisababishia mateso na kufanya chochote kwa watu hawa. (766). 


Sala: Ee Upendo kamilifu, tawala moyo wangu nisaidie nifanye yakupendezayo kwa imani yote. (328).



12. KITUO CHA KUMI NA MBILI - YESU ANAKUFA MSALABANI

Somo: Yn 19:33-40


Yesu kwa Mt. Faustina:  Haya yote ni kwa ajili ya ukombozi wa Roho zetu. Kumbuka ee binti yangu unachofanya kwa ajili ya kuwakomboa (1184). 


Mt. Faustina: Ndipo nikamuona Bwana Yesu kapigiliwa misumari juu ya msalaba. Akiwa amening'inizwa niliona roho nyingi ajabu zikiwa zimening'inizwa msalabani kama yeye. Baadae nikaona kundi jingine kubwa la roho na pia kundi la tatu. Kundi la pili lilikuwa halijagongwa misumari msalabani ila walikuwa wameshikikia kwa nguvu misalaba mikononi mwao. Kundi la tatu lilikuwa haligongwa misumari wala hawakuwa wameshikilia misalaba mikononi Bali wanaivuta kwa nyumà.


Yesu kwa Mt. Faustina:  He! Unaona hizi roho? Wale ambao wanateseka nami kwa uchungu, pia uchungu wao utakuwa kama wangu katika utukufu. Pia wale ambao hawana uchungu hawafanani kama mimi watapata fiada ndogi katika utukufu wangu. (446). 


Sala: Yesu mkombozi wangu, nifiche ndani ya moyo wako, nineemeshe kwa rehema zako ili niweze kufanana nawe katika uoendo wa msalaba nishiriki katika utukufu wako.



13. KITUO CHA KUMI NA TATU - YESU ANASHUSHWA MSALABANI

Somo: Lk 23:47-49 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Kipenzi changu ni roho ambayo inaamini wema wangu na moyo huo umeweka matumaini kwangu. Kwa moyo mkunjufu kabisa na bila yoga wowote, nitaujalia kila unachokiomba. (453). 


Mt. Faustina:  Nakimbilia huruma yako, Mungu Wa Rehema na huruma, wewe mwenyewe ndiye mwema. Japokuwa uovu wangu nimkubwa mno, na matendo yangu maovu ni mengi, nakutumainia wewe bwana kwani wewe ni Mungu wa Huruma na tangu miisho ya ulimwengu haijawahi kusikika ukimtelekeza MTU yoyote anayekutumainia. (1730). 


Sala: Yesu mwenye huruma, nakuomba uniongezee moyo wa kukuamini wewe na niweze kutoa ushuhuda Juu ya matendo yako mema na upendo wako.



14. KITUO CHA KUMI NA NNE - YESU ANAZIKWA KABURINI

Somo: Yn 19:38-42 


Yesu kwa Mt. Faustina:  Lakini mwanangu, bado hujafika nyumbani, nenda ukamee kwa Neema zangu, na upiganie ufalme wangu kwenye mioyo ya watu. Pigana kama mwana Wa mfalme afanyavyo, ukikumbuka siku za utumwa wako zitapita kwa haraka sana na uwezekano Wa kuupata ufalme Wa Mungu ukiwa ni  mkubwa mno. Nategemea toka kwako, mwanangu, nyoyo nyingi zitatukuza huruma yangu milele. (1489). 


Mt. Faustina:  Kila nyoyo uliyonipa, nitajitahidi kuziombea na kuzilinda kwa sala, ili huruma yako ifanye kazi nadani yao. Ee Yesu mpenda roho zetu, nashukuru kwa kunipa ushujaa huu Wa kuzielekeza nyoyo za binadamu wenzangu kwako. (245). 


Sala: Nijalie, huruma ee bwana, ili pasipotee roho yeyote uliyo nikabidhi kwa ajili yako.               



SALA YA MWISHO

Yesu wangu, tegemeo langu pekee, nashukuru kwa hiki kitabu ulichonifunulia kwenye macho ya mioyo yangu. Kitabu hiki ni safari yako ya mateso katika njia ya msalaba ulioubeba kwa ajili ya upendo wako kwangu ee Yesu wangu. Kupitia kitabu hiki nimejifunza kumpenda Mungu na Roho. Kitabu hiki kimejaa hazina zisizoharibika. Ee Yesu tunaona ni roho chache zinazotambua na kuelewa kufia dini kwako kwa upendo mkubwa. Ni heri nyoyo zilizotambua upendo wa Yesu kwetu Wa kutukomboa.


KWA AJILI YA NIA ZA BABA MTAKATIFU 


Baba Yetu....Salamu Maria....Atukuzwe.... 



SALA KWA HESHIMA YA MSALABA MTAKATIFU:

Baba Mungu Mwenyezi, kwa heshima kwako mwanao mpenzi alikubali kifo cha msalaba kwa ajili ya ukombozi Wa mwanadamu. Tunatambua fumbo la msalaba kwetu. Tusaidie tupate zawadi hii ya ukombozi Mbinguni. Tunaomba haya yote kwa njia ya mwanao Yesu Kristy, anayeishi na kutawala pamoja Nate, Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu milele na milele.  Amina.

No comments:

Post a Comment