MASOMO
YA MISA, JANUARI 16, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 1 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
4:12 – 16
Neno
la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na ivungo na mafuta
yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala
hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na
kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.
Basi,
iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na
tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana
nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi
katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa
ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:7 – 9, 14 (K) Yn. 6:63
(K)
Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako.
Ee
Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako,
Na
wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.
Umempa
haja ya moyo wake,
Wala
hukumzuilia matakwa ya midomo yake. (K)
Maana
umemsogezea Baraka za heri,
Umemvika
taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Alikuomba
uhai, ukampa,
Muda
mrefu wa siku nyingi, milele na milele. (K)
Utukufu
wake ni mkuu kwa wokovu wako,
Heshima
na adhama waweka juu yake.
Maana
umemfanya kuwa Baraka za milele,
Wamfurahisha
kwa furaha ya uso wako. (K)
SHANGILIO
Lk.
4:18 – 19
Aleluya,
aleluya,
Bwana
amenituma kuwahubiri maskini habari njema, kuwatangazia wafungwa kufunguliwa
kwao.
Aleluya.
INJILI
Mk.
2:13-17
Yesu
alitoka, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha. Hata
alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia,
Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Hata
alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi wa wenye dhambi
waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata.
Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye
dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na
wenye dhambi? Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali
walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment