“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Januari 16, 2021,
Juma
la 1 la Mwaka wa Kanisa
Ebr
4: 12-16;
Zab
18: 8-10, 15;
Mk
2: 13-17
KUMLETA
YESU KWA “WASIOMTAMANIKA”!
Karibuni
sana ndugu zangu kwa tafakari ya neno La Mungu asubuhi ya leo katika adhimisho
la Misa Takatifu. Leo tafakari yetu inaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo
wa katikati na hapa tunakutana na ujumbe usemao: neno lako ee Bwana ni roho na
uzima.
Neno
hili linauwezo wa kumtia mjinga hekima. Na hakuna yeyote mwenye kuyatii maneno
na kupotea. Ni lazima yatamuokoa tu. Somo la kwanza linaendeleza ukuu wa neno
la Mungu kwa kusema kwamba neno hili linanguvu na ukali kama upanga mkali. Na
mbele ya neno hili, kila kitu kinakuwa wazi-hakuna kinachofichika.
Huu
ndio ukuu wa Mungu ndugu zangu, kwake yeye hatuwezi kuficha kitu, na yeye
hapendi dhambi. Shukrani kwa Yesu. Yeye ndiye aliyekuhani mwenye kutuombea
mbele ya Mungu. Kweli tukienda mbele ya Mungu bila Yesu kutuombea, hakika
nafasi yetu ni finyu. Yesu yupo. Tumwangukie nasi tutaweza kumfikia Baba.
Tusiache kumwamini Yesu hata siku moja.
Somo
letu la injili linatuhimiza kuanzisha urafiki na Yesu ili tupate okolewa. Leo
Lawi anaanzisha naye urafiki na hakika anafaidi sana. Anapatwa kufundishwa juu
ya dhambi zake na kama tutaendelea kusoma hii sehemu ya injili, tutagundua
kwamba Lawi alichomwa na Yesu na hata kudiriki kurudisha kile alichodhulumu.
Huyu ndiye Yesu kuhani wetu. Hakika anatupenda sana. Anapokutana na watoza
ushuru na makahaba, hawafukuzi, anawaalika, kwani Yesu anajua hali yao lakini
taratibu wao wenyewe wanaanza kubadilika na kuacha maisha yao ya zamani kama
wanavyofanya akina Mathayo (Lawi) leo.
Sisi
nasi tuwe na upendo kwa wenzetu hata wale waliotukosea. Tutambue kwamba Bado ni
viumbe vya Mungu na tuwasaidie kumrudia Mungu.
Tusitangaze
dhambi ya yeyote, mlete kwa Yesu naye atabadilishwa kama Lawi anavyobadilishwa
leo. Tusiogope kukiri makosa yetu mbele ya Yesu, yeye anatufahamu sisi mno,
tuwe wazi kwake atufanye upya.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment