“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa,
Januari 15, 2020,
Juma
la 1 la Mwaka wa Kanisa
Ebr
4: 1-5, 11;
Zab
77: 3-4, 6-8;
Mk
2: 1-12
WAKATI
MUNGU AKIWA KIMYA
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo katika adhimisho la
Misa Takatifu. Leo neno la Bwana katika Zaburi yetu ya wimbo wa katikati,
mzaburi anasisitiza kwamba tusiyasahau matendo ya Mwenyezi Mungu kamwe.
Tusisahau
na maajabu yake, yote. Yafaa yasimuliwe kwa vizazi vijavyo na kamwe tusiige
ukaidi kama ule walionesha baadhi ya wazee wa taifa la Israeli. Ukaidi wao
uliomfanya Mungu asiheshimike na vizazi vijavyo.
Somo
letu la kwanza linatukumbusha juu ya uwepo wa pumziko lililoandaliwa na Bwana-na
kwenye kulipata pumziko hili, bado hatujachelewa. Tunaaswa kwamba ikiwa
tutakumbatia moyo wa ukaidi, hakika tutashindwa kulipata pumziko hili. Wazee wa
taifa la Israeli walipoonyesha ukaidi, walishindwa kufika katika nchi ya ahadi
na kupata pumziko. Waliishia kufa jangwani kwa sababu ya kuifanya migumu mioyo
yao.
Sisi
tukija kwa Bwana tusifanye migumu mioyo yetu, tukija kwa Bwana lazima tuyeyuke
kama nta mbele ya moto, lazima tuanguke kifudifudi tukitambua kwamba hakuna
kama yeye. Ukaidi wetu na majivuno vitatukosesha mengi.
Katika
injili yetu, tunakutana na waandishi wakiifanya migumu mioyo yao, hawataki
kuifungua na kuona muujiza uliofanywa na Yesu. Wanakataa pia kuona imani na
maumivu ya mgonjwa. Wanaishia kutafuta makosa toka kwa Yesu. Hapa waliifanya
migumu mioyo yao na hakika wasingaliweza kumwamini au kupewa pumziko na Bwana
Yesu.
Sisi
ndugu zangu tusioneshe ukaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Wengi tunalisubiri hili
pumziko litutulize. Ulimwenguni tunateseka lakini tunategemea kwamba ipo siku
tutaokolewa na Bwana Yesu na kupewa hilo pumziko ikiwa tutaendelea kuilainisha
mioyo yetu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment