MASOMO
YA MISA, DESEMBA 6, 2020
DOMINIKA
YA 2 YA MAJILIO MWAKA B
MWANZO:
Isa.
30:19, 30
Enyi
watu wa Sayuni, Tazameni Bwana atakuja kuwaokoa mataifa; naye Bwana
atawasikilizisha sauti yake ya utukufu katika furaha ya mioyo yenu.
SOMO
1
Isa.
40:1-5, 9-11
Watulizeni
mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu,
kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umechiliwa;
kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dahmbi zake zote.
Sikiliza,
ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani
njia kuu kwa Mungu wetu, Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima
kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa;
Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa
kinywa cha Bwana kimenena haya.
Wewe
uuhubiriye Sayuni habari njema, panda juu yam lima mrefu; Wewe uuhubiriye
Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope;
Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.
Tazameni,
Bwana Mungu atakuja kama shujaa, na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni,
tahawabu yake I pamoja naye, na ijara yake I mbele zake.
Atalilisha
kundi lake kama mchungaji, atawakusanya wanakondoo mikononi mwake; na
kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
85:8-13 (K) 7
(K)
Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, utupe wokovu wako.
Na
nisikie atakavyosema Mungu Bwana,
Maana
atawaambia watu wake amani,
Hakika
wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu
ukae katika nchi yetu. (K)
Fadhili
na kweli zimekutana,
Haki
na amni zimebusiana.
Kweli
imechipuka katika nchi,
Haki
imechungulia kutoka mbinguni. (K)
Naam,
Bwana atatoa kilicho chema,
Na
nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki
itakwenda mbele zake,
Nayo
itazifanya hatua zake kuwa njia. (K)
SOMO
2
2Pet.
3:8-14
Wepenzi,
msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka
elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine
wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia
kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. Lakini siku
ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo
makuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo
ndani yake zitateketea.
Basi,
kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia
gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya
Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na
viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake,
tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. Kwa hiyo,
wapenzi kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidi ili mwonekane katika amani
kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Lk.
3:4, 6
Aleluya,
aleluya,
Itengenezeni
njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake. Na wote wenye mwili watauona wokovu wa
Mungu.
Aleluya.
INJILI
Mk.
1:1-8
Mwanzi
wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama ilivyoandikwa katika nabii
Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia
yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni
mapito yake.
Yohana
alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la
dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa yerusalemu wote, wakabatizwa
katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa
za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi
kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Akahubiri akisema, Yuaja nyuma
yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza
gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa
Roho Mtatifu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment