“MBEGU
ZA UZIMA”
Desemba
6, 2020.
------------------------------------------------
DOMINIKA
YA 2 LA MAJILIO
Somo
la 1: Is 40:1-5, 9-11 Mungu anamwambia Isaya awafariji watu wake, lakini pia
anawaambia waandae njia kwa ajili ya ujio wa Bwana, Mungu anakuja kuwaokoa watu
wake
Wimbo
wa katikati: Zab 84:9-14 Bwana ni mwenye huruma, sauti yake inaongea Amani, na
msaada wake ni kwa wale wote wanao mtii. Kwake huruma na uaminifu nimekutana,
haki na Amani vimekumbatiana.
Somo
la 2: 2Pet 3:8-14 kama Paulo, Petro anaamini kwamba Yesu atakuja muda sio
mrefu, wakati usiotarajiwa, hivyo wote wanapaswa kujiandaa. Kama Bwana anakawia
kuja, ni kwasababu anawapa watu muda wakutubu na kuwa tayari kukutana naye
atakapokuja.
Injili:
Mk 1:1-8 Marko anafungua injili yake kwa taswira ya Yohane akitangaza umuhimu
wa watu kutubu na kubatizwa kwa ajili ya ujio wa Masiha anayekuja katika maisha
yao.
------------------------------------------------
MAJILIO:
ANDAA NJIA YA BWANA
Mtu
mmoja alikuwa na saa kubwa ya gharama sana iliyotengenezwa Switzerland.
Aliiweka dirishani, sehemu ambayo ilionekana na wote waliokuwa wakipita njia na
wengi walirekebisha majira ya saa zao kwa kutazama saa hii. Lakini siku moja
saa ilipata shida Fulani. Ilianza kuonyesha saa ambayo sio. Hivyo mwenye saa
kila siku alitumia nguvu nyingi na muda mwingi kuwa karibu na saa ili aiweke
kwenye wakati unaotakiwa. Hali hii iliendelea kwa miaka. Siku moja mtu
alimfuata akamwambia kwanini “badala ya kutumia nguvu nyingi na muda wako
mwingi kuweka saa hii kwenye wakati sahihi kila siku, kwanini usirekebishe
vifaa vya ndani?” Yule mwenye saa alifurahi kwani hakuwahi kufikiri hivyo. Sisi
nasi tuonaogopa kubadilika kutoka ndani kwani tunaogopa kuonakana vibaya
machoni pa watu au pengine tutapoteza umaarufu wetu kwasababu watu wameshatuona
kama watu wenye saa ya gharama hivyo tunafanya kila jitihada umaarufu wetu
usipotee, na hivyo tunateseka kweli. Kwanini tusibadilike kutoka ndani na
kuanza kufurahia maisha kama yalivyo?
Mungu
hakumtuma Mwanae aje abadili watu wachache. Alimtuma Mwanae awabadili watu wote
na ubinadamu wote. Ndio maana kila majilio tunakutana na Yohane Mbatizaji
akitutangazia ujio wa ukombozi wa wanadamu wote. Anawaambia watu “kuanda njia
kwa ajili ya ujio wa Bwana”. Lakini kwanini tunahitaji kujiandaa kwa jili ya
Bwana?
Siku
moja mtu mmoja alivyutwa na jagi nzuri aliloona sokoni. Alilinunua na kwenda
nalo nyumbani. Baada ya kuliweka sebuleni na kutazama nyumba yake alitambua
kwamba lile jagi lake lilikuwa nzuri sana kuliko nyumba yake na hivyo akaamua
kupaka rangi nyumba yake. Na kununua kateni nzuri za rangi zuri, na kununua
makochi na kupendezesha nyumba yake. Kwa njia ya jagi lile nyumba nzima
ilibadilika na kuwa nyumba mpya. Wakati Yesu anapo ingia katika maisha yetu
anabadili kila ktiu. Kila kitu ambacho kinahitaji kubadilika kitaonekana
dhahiri. Tunapo sogea karibu zaidi na Mungu ndivyo tunavyozidi kujiona tulivyo
na kuona utofauti wetu! Na hii ndio maana tunayohitaji kuandaa njia kwa jili ya
Bwana.
Majilio
ni kipindi cha kungojea ujio wa Bwana, na Bwana pia anatusubiri kurudi kwetu
kutoka kwenye dhambi. Mungu wetu anatupenda sisi na upendo wake unatufanya sisi
tumtafute yeye. Mungu alienda kuwatafuta adamu na Eva katika bustani ya edeni,
wakati wakiwa wamejificha, walijificha baada ya kujua kwamba wameenda kinyume
na kazi ya Mungu. Wakati mwingine sisi tunalalamika Mungu amejificha mbali na
uso wetu, na kwamba haonekana lakini katika hali ya kweli sisi ndio
tuliojificha kutoka kwake? Na hivyo Mungu akauliza swali: “upo wapi” ni Mungu
mwenyewe aliye anza kutafuta, kwa upendo wake kwetu. Agano lote la kale
ameendelea kumtafuta Mwanadamu na kumleta kwenye upendo wake. Je, tupo tayari
kumkaribsha yeye katika maisha yetu?
Katika
somo la kwanza tunasikia kwamba “andaa njia katika jangwa, Bwana anakuja. Fanya
njia iliyo nyooka Bwana wetu anakuja”. Ni katika mioyo yetu tunapaswa kufanya
njia iliyo nyooka kwa ajili ya Mungu. Ni mabonde ya dhambi katika mioyo yetu
yanapaswa kusawazishwa kwa huruma na uponyaji wa Mungu, na vilima vya majivuno
ndani ya mioyo yetu ambavyo vinapaswa kusawazishwa. Somo la pili linatukumbusha
kwamba tunaishi katika kipindi cha huruma, wakati tukiwa na muda wa kutubu.
Yohane Mbatizaji kama Isaya anasema “ tengeneza njia ya Bwana” “tengeneza njia
iliyo nyooka” maisha ya dhambi na vishawishi yaachwe. Sawazisha vilima vya
ubinafsi na kujaza mabonde ya utupu kwa sala na fadhila. Njia zisizo nyooka
zinapaswa kunyooshwa kwa ukarimu na kujali.
Maandalizi
yetu ni muhimu tuangalie mioyo yetu na kumkaribisha Mungu katika maisha yetu,
na uponyaji wake ili Roho Mrtakatifu atufanye viumbe vipya. Toba inaanza kwa
kutambua umuhimu wa kumpokea Mungu, kwa kujitazama sisi ni nani na tupo kwa
ajili ya nini, pia kutazama jitihada zetu za kumfuata Kristo. Ni kutambua uhaba
wetu wa kiroho na kumfuata Yesu mkombozi wetu, na ambaye anatupatia nguvu ya
kukuwa katika mapendo. Noeli itakosa maana kama hatutaandaa njia katika mioyo
yetu kwa ajili ya Bwana. Wakati huu wa majilio, tujiulize hivi ni dhambi gani
inaniweka mbali na Mungu? Tuuungame na kufanya toba ili upendo wa Mungu utukute
sisi.
Sala:
Ninakushukuru Bwana, kama Mchungaji mwema unatulisha sisi, unatukusanya kama
Mchungaji ukituchukua kifuani pako kwa uangalifu. Njoo Bwana Yesu! Ninatamani
kubaki katika mikono yako kwa milele yote. Bwana, tunaomba tuone ukarimu wako,
tujalie ukombozi wako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment