“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 5, 2020.
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 1 LA
MAJILIO
Somo la 1: Isa 30:19-21,
23-26 Mungu ni mwingi wa neema kwa wanao mwita, mara anaposikia hukujibu. Mungu
ataviunga vidonda vya watu wake na kuponya jeraha walizo umizwa.
Wimbo wa Katikati: Zab
146:1-6 Mungu anaujenga Yerusalemu na kuwarudisha Waisraeli kutoka utumwani.
Ataponya mioyo iliovunjika, na kufunga vidonda vyao. Wana heri wanao mtumaini
Bwana.
Injili: Mt 9:35 – 10:1,5,
6-8 kwa kuvutwa na huruma ya watu waogonjwa, Yesu anawaamuru mitume wake
wachukue kazi yake ya kuponya na kuwafariji watu.
------------------------------------------------
TUMWACHE MUNGU ATUANDIKIE
HISTORIA MPYA
Mpango wa Mungu
unatusogeza mbele bila kuturudisha nyuma. Tunaweza tu kusogea mbele kwa fadhila
au kurudi nyuma kwa kutenda dhambi. Kama hatufanyi ili viendane na Ufaleme wa
Mungu basi uwepo wetu hauna maana. Maisha yetu yanakosa utaratibu. Katika
Biblia, Mungu ameingia katika maisha ya mwandamu ili kumleta karibu na mapenzi
yake. Anatutegemea sisi tuchukue jukumu, kumgeukia na kuchagua njia nyemembamba
ambayo haipitwi na wengi na kufuata njia yake ambayo wakati mwingine tunaweza
tusiione kama tunavyotaka wenyewe, Neno lake. Huu ndio muda wa kujitakasa-muda
ambao tupo jangwani.
Leo katika liturjia yetu
ya kipindi cha majilio, tunaomba kwa ujio wa Mwana wa Mungu, tukijua pia
alishakuja, tunaye pamoja nasi. Tunatumaini katika kile ambacho yeye anacho.
Hatuwezi kutosheka kwakusema hatumuhitaji Yesu kwa uponyaji, huruma yake ya
kutugusa. “kwa kuwaona makutano aliwahurumia” na leo hii hatuna sababu ya
kusema kwamba huruma yake imeisha kwetu. Anaendelea kuponya mioyo iliyo umizwa
na kufunga vidonda vyao. Anauwezo wa kutuambia idadi ya nyota na kuzipa kila
moja jina. Injili inatuambia kwamba aliwatuma wale mitume kumi na mbili na
kuwapa mamlaka ya kuponya na kuondoa pepo wabaya na kuponya magojwa ya kila
aina, “kuponya wagonjwa, kufufua wafu, na kufukuza pepo. Mmepewa bure toeni
bure”. Mamlaka haya hayaja ondolewa ndani ya kanisa na watu wake.
Katika somo la kwanza
tunasikia pia: “hata ugeuke kushoto au kulia au nyumba utasikia sauti
ikikuambia “Njia ni hii ifuate”. Nabii anawapa uhakika watu kwamba kama
watamtafuta Mungu kwa hakika watampata-njia ni hii ifuate”!. Mpaka tuisikia
hiyo sauti na kuifuata, hatuwezi kuwa huru mpaka tumeifuata sauti hiyo. Ni
kitendo cha kubadili mtazamo wetu na kuchagua kuyafuata mapenzi ya Mungu, bila
kujali gharama yake! Sisi sote tunafanya makosa katika maisha. Wengi wetu
tunapoteza mwelekeo tukiwa njiani. Tunapaswa kurudi na kusikiliza sauti ya
Mungu ndani mwetu. Wakati Mungu anatamani kuingia katika maisha yetu, tunapaswa
kufanya njia iwe imenyooka ili yeye aweze kuingia ndani.
Sala; Mungu mwenye
huruma, tunaomba Ekaristi tunayopokea na liturjia tunayo adhimisha ituletee
msaada wa neema yako, tuweke huru kutoka katika dhambi zetu, na utuandae kwa
kuzaliwa kwa Mkombozi wetu. Yesu nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment