MASOMO
YA MISA DESEMBA 11, 2020
IJUMAA,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
48:17-19
Bwana,
mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi: Mimi ni Bwana, Mungu wako,
nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti
ungalisikiliza amri zangu! Ndipo Amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na
haki yako kama mawimbi ya bahari; tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na
hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingali katika,
wala kufutwa mbele zangu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
1:1-4,6 (K) Yn. 8:12
(K)
Akufuataye, Bwana, atakuwa na nuru ya uzima.
Heri
mtu yule asiyekwenda,
Katika
shauri la wasio haki,
Wala
hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala
hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali
sheria ya Bwana ndiyo impendezayo,
Na
sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K)
Naye
atakuwa kama mti uliopandwa,
Kandokando
ya vijito vya maji.
Uzaao
matunda yake kwa majira yake,
Wala
jani lake halinyauki;
Na
kila alitendalo litafanikiwa. (K)
Sivyo
walivyo wasio haki,
Hao
ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Kwa
kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki,
Bali
njia ya wasio haki itapotea. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Bwana
atakuja, nendeni kumlaki, Yeye ni mfalme wa Amani.
Aleluya.
INJILI
Mt.
11:16-19
Siku
ile, Yesu aliwaambia makutano: Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki?
Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema, Tuliwapigia
filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.
Maana
Yohane alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo. Mwana wa Adamu alikuja,
akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na
wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment