“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba
11, 2020.
------------------------------------------------
IJUMAA,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
Somo
la 1: Isa 48:17-19 Bwana anatuambia, kama tungefuata na kuonywa na amri zake,
furaha yetu ingekuwa kama mto, uaminifu wetu kama mawimbi ya bahari.
Wimbo
wa katikati: Zab 1:1-4, 6 Anayenikufuata wewe Ee Bwana, atakuwa na uzima wa
milele. Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya mto, unaozaa matunda yake kwa
wakati.
Injili:
Mt 11:16-19 Yesu analalamika kuhusu unafiki wa Mafarisayo na Waandishi. Si yeye
wala Yohane ambaye ataweza kukata kiu ya watu ambao wana aina ya Masiha wao
wanaompenda wao, mwenye kutimiza haja ya njia zao.
------------------------------------------------
WOTE
WANAALIKWA KWENYE MEZA YA YESU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
katika somo la kwanza Bwana Mungu anamueleza Yuda kwamba angalau kama
angalifahamu faida iliyopo katika kushika sheria zake. Hakika angalijikuta
mahali pa pekee zaidi, asingalikuwa katika shida hizo, angalikuwa mkuu kabisa.
Israeli
alikuwa maskini kwa sababu alienda kuiga mataifa mengine, alikwenda kuiga ya
dunia na kula huko mataputapu na mwisho wa siku akajikuta katika shida kubwa
namna hii, ambapo hawezi kabisa kujiletea ukombozi.
Ndugu
zangu kumcha Bwana kuna faida kubwa sana. Wengi wetu tupo katika hali mbaya kwa
sababu tuliacha kumcha Bwana, tukaiga ya dunia, tukaiga watu maarufu, tukaiga
wanamuziki, tukataka kuvaa wanavyovaa, wanavyoongea, wanavyoimba, wanavyooa na
kuolewa, tukaiga mitindo yao ya maisha na kudharau maisha ya sala kama
yaliyopitwa na wakati.
Sala
ndugu zangu haijapitwa na wakati, huku kwenda na wakati ndiko kunakoturudisha
nyuma. Mara nyingi tukishafanikiwa huwa tunamsahau Bwana, ni wakati tu wa shida
ndio tunamrudia Bwana. Naamini kama wakati wa mafanikio tungaliendeleza kukaa
na Bwana katika sala, tungalisalia kukua zaidi. Mara nyingi mafanikio
yanatukosesha ukaribu na Mungu na hapa ndipo tunaanguka zaidi.
Tumwombe
Mungu neema ya kumrudia hata kipindi cha mafanikio. Tuyatunze mafanikio yetu
kwa njia ya sala.
Katika
somo la injili Yesu anasononeshwa na vizazi hivi vya sasa kwa sababu havikosi
majibu mabaya na kuwatungia wengine mabaya. Kilimuona Yohane kikamuona anapepo,
Yesu anaitwa mlafi. Hiki ni kizazi chenye wivu, kisichotaka mtu anayewapa
changamoto. Kinatafuta kumwangusha kila mtu ili basi wote waonekane wameoza ili
asitokee wa kuwakaripia wanapofanya ubaya.
Tabia
hii ikiendelezwa ulimwenguni huishia kuufanya urudi nyuma, na tunaishia kukosa
watakatifu, tukitaka kila mtu awe mbaya. Sisi tukiona mtu anayejitokeza na
kuishi vyema tumtie moyo, tusitake kila mmoja arudi nyuma afafane na sisi, awe
na matope kama sisi ndio tuone ati ni vyema. Hapana, ukimuona anayejitahidi
kuwa mtakatifu mpatie moyo. Usitafute mapungufu yake na kuyatangaza.
Ndivyo
inavyofanywa na vyombo vya habari sasa vya ulaya. Yaani inaweza kufika mahali
wanalitangaza kanisa vibaya ili lisionekane kama lina utakatifu wowote.
Lionekane kama "NGO" tu. Tunakosa watakatifu kwa sababu ya kusemana
vibaya. Wale wanaojitahidi tunawavuta chini. Sisi tuwatie wengine moyo
wajitaidi zaidi na zaidi. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment