MASOMO YA MISA,
NOVEMBA 29, 2020
DOMINIKA YA 1 MAJILIO
MWAKA
MWANZO:
Zab. 25:1 – 3
Ee Bwana, nakuinulia
nafsi yangu, Ee Mungu wangu, nimekutumaini wewe, nisiaibike, adui zangu
wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja.
SOMO 1
Isa. 63:16-17; 64:1, 4-8
Wewe, Bwana, ndiwe Baba
yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. Ee Bwana, mbona umetukosesha
njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili
ya watumishi wako, kabila za urithi wako. Laiti ungepasua mbingu, na kushuka,
ili milima iteleme mbele zako. Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia,
wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo
kwa ajili yake amngojaye.
Wwe wamlaki yeye
afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako;
tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya
muda mwingi; nasi, je! Tukaokolewa?
Kwa maana sisi sote
tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo
iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama
upepo uondoavyo. Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa
kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu. Lakini sasa,
Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu
kazi ya mikono yako.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 80:1-2, 14-15, 17-18
(K) 3
(K) Ee Mungu, uturudishe,
uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
Wewe uchungaye Israeli
usikie,
Wewe uketiye juu ya
makerubi, utoe nuru.
Uziamshe nguvu zako.
Uje, utuokoe. (K)
Ee Mungu wa majeshi,
tunakusihi, urudi,
Utazame toka juu uone,
uujilie mzabibu huu.
Na mche ule ulioupanda
Kwa mkono wako wa kuume;
Na tawi lile ulilolifanya
Kuwa imara kwa nafsi
yako. (K)
Mkono wako na uwe juu
yake
Mtu wa mkono wako wa
kuume;
Juu ya mwanadamu
uliyemfanya
Kuwa imara kwa nafsi
yako;
Basi hatutakuacha kwa
kurudi nyuma;
Utuhuishe nasi tutaliitia
jina lako. (K)
SOMO 2
1 Kor. 1:3-9
Ndugu zangu, neema na iwe
kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Namshukuru Mungu sikuzote
kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa
kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa
yote; kama ushuda wa Kristo ulivyothibita kwenu; hata hamkupungukiwa na karama
yoyote, mkikutazamaia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye
atawathitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa nay eye mwingie katika ushirika wa Mwanawe,
Yesu Kristo Bwana wetu.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
SHANGILIO
Zab. 85:7
Aleluya, Aleluya,
Ee Bwana utuonyeshe
rehema zako utupe wokovu wako,
Aleluya.
INJILI
Mk. 13:33-37
Siku ile: Yesu aliwaambia
wafuasi wake: Angalieni, kesheni, (ombeni), kwa kuwa hamjui wakati ule
utakapokuwapo. Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameicha nyumba yake,
amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu
akeshe. Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni,
au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili
ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment