“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Novemba 28, 2020
Juma
la 34 la Mwaka wa Kanisa
Ufu
22:1-7;
Zab
94:1-7;
Lk
21:34-36
KUWA
TAYARI NA SALI!
Siku
ya leo masomo yanatualika kuwa tayari daima, kuwa makini na pia kusali daima.
Yesu leo anatupa ujumbe huo huo alivyo ulizwa kuhusu ujio wa Ufalme wa Mungu
(Lk 17:20-21). Ujio wa Ufalme wa Mungu utakuja kama radi, bila kutegemewa, bila
kuwa na kiashirio kabla. Tunapaswa kuwa makini na kujiandaa. Kusubiri kukiwa
kurefu sana, kuna hatari ya kujisahau na kupoteza muelekeo. Yesu anatuonya hapa
kwa vitu vitatu, kujikita kwenye anasa na kuwa na ulafi, ulevi, na kusumbukia
kwa kuwa na mashaka ya maisha haya. Tunapaswa kuwa tayari na kuwa makini “ili
siku hiyo isije ikatushika kama mtego”, ukumbusho kwamba Mungu hapendi hata
mmoja wetu apotee. Sala inatupa matumaini, inatufanya tuwe tayari, inazima
tamaa zetu na kutupa nguvu ya kuendelea kuishi katika neno la Mungu. Inasaidia
pia waamini kusimama tukiwa tumejiandaa mbele ya Mwana wa Adamu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment