“MBEGU
ZA UZIMA”
Novemba
29, 2020.
------------------------------------------------
DOMINIKA
YA KWANZA YA MAJILIO
Somo
la 1: Isa 63:16-17, 64:1,3-8 Wakati fulani katika mwaka wakati majani machache
tu yamejishika kwenye matawi, Isaya alilia nakusema "Tumekauka kama majani
ya miti, na uchungu wetu unatupeperusha kama upepo". Anasali kwa Mungu kwa
ajili ya jina la watu wake, akiomba msamaha kwa ajili ya dhambi za watu na
kuweka roho zao katika mikono ya Mungu.
Kiitikio.
Zaburi: Zab 80:2-3,15-16,18-19 Jikabidhi kwa Mungu. Mpokee yeye katika maisha
yako leo. Lia kwa nguvu pamoja na mzaburi, "utuangaze uso wako nasi
tutakuwa salama"
Somo
la 2: 1 Kor 1:3-9 Paulo anasikika akiwa na matumaini licha ya matatizo huko
Korintho kwasababu imani yake si kwa ajili ya uwepo wa Wakorintho bali ipo kwa
Mungu Baba ambaye ni mwaminifu kwa ahadi zake. Paulo anaongea kuhusu hili
kutaka kuwaonesha Wakorintho kwamba neema ya Mungu inatosha kubadilisha maisha
yao kutoka katika dhambi zao na kumgeukia yeye ambaye amejaa ukweli.
Injili:
Mk 13:33-37 Yesu "anatuita sisi". Mfuasi anapaswa kuwa makini kila
wakati, kwani hajui siku ya ujio wake.
------------------------------------------------
MAJILIO:
KUWA TAYARI, KUWA MAKINI
Kanisa
lina nyakati mbali mbali. Vipindi mbali mbali kukumbuka ukombozi wa Mungu,
upendo wakujitoa. Katika kipindi hiki kanisa linatufundisha katika hali ya
undani, kutoa nyakati za kuongeza imani, ili tukiwa tumejiandaa tunampa Bwana
nafasi ya kujitoa kwetu katika hali ya ukamilifu kwetu.
Majilio
ni Kipindi maalumu cha kujiandaa kwa ajili ya sherehe ya Noeli. Majilio maana
yake ujio au "kuja", maandalizi ya ujio wa Mfalme. Kiliturjia, ni
maadhimisho ya kipindi kilichopita, historia ya kuzaliwa Yesu. Kuzaliwa kwa
Yesu kama Mwanadamu tayari imeshatokea. Maandalizi yetu hayapo kama yale ya
Waisraeli wanaosubiri wakati ujao. Lakini kama Israeli mpya, tunaishi wakati
ujao kwa uhakika wa kuzaliwa Bwana, na pia kwa ujio wake wa sasa. Maisha yetu
yote ni Majilio, wakati ambao Bwana atakuja. Ingawaje ameshakuja kwa kila mmoja
wetu, hajaja katika ukamilifu wote. Tunajilinganisha na wale wa zamani
waliokuwa wanamsubiri Bwana. Kwa kuingia katika hali yao, tukijenga matamanio
yetu kama ya kwao, matumaini yao, tunasukumwa kutamani ujio wao zaidi na zaidi,
tunajitakasa na kujiandaa kwa ujio wake.
Tukiwa
tunajiandaa katika hali ya Sakramenti, Bwana anakuja, Kanisa linatangaza, andaa
moyo wako kwa ujio wake, hatufanyi kama maigizo bali tunafanya kwa moyo kabisa
ndani ya Liturjia. Bwana anakuja katika hali ambayo hajawahi kuja kabla.
Tunaingia katika mafumbo ya majilio tukiwa na imani thabiti, tukiwa na shauku,
kutamani, tukiamini kwamba Mungu anajitoa kwetu katika hali ambayo hajajitoa
tena kabla. Atakuja, tunatazamia tukiwa na mapendo makuu.
Jaribu
kufikiri kwa mfano unashanga unamkaa asubuhi na leo ni Noeli alafu umesahau
kuandaa! Huna chakula, hujaandaa nguo, wala hujapamba kitu, na huna mpango
unaoeleweka. Bilashaka hatuwezi kuruhusu ali hiyo itokee. Mara nyingi
hatujiandai kusherekea vizuri kuzaliwa kwa Yesu katika mioyo yetu. Kipindi cha
Majilio ni kipindi cha kujiandaa kumkaribisha tena Yesu ndani ya mioyo yetu.
Ni
kwa kuwa na moyo wa unyenyekevu ulio makini. Mchezaji mzuri wa mpira ni yule
aliyeweka mawazo yake katika ule mpira na wachezaji wenzake. Mwanafunzi mzuri
ni yule anayeweka mawazo yake darasani na kusikiliza anacho fundisha mwalimu.
Mkatoliki mzuri ni yule aliyeweka mawazo yake ya roho na mwili kumwelekea
Mungu, akijiingiza kwenye sala daima na kufanya matendo ya huruma. Tunatambua
kuwa Noeli itakuja tarehe 25, mwezi wa 12. Tutakuwa tunaimba nyimbo mbali
mbali, kanisa na mazingira yetu yatapambwa vizuri na nyota na maua mbali mbali,
watu watanunua nguo mpya. Yote haya ni mazuri. Lakini uwepo wa Kristo
tusiuchukulie katika hali hii tu. Yeye anakuja katika hali ya ukimya wa roho
zetu ili tuweze kukuwa naye katika mioyo yetu! Tunapaswa kujiandaa kwa kuungama
dhambi zetu vizuri na kutakasa roho zetu. Lakini pia lazima kutambua kuungama
tu ya zamani sio alama ya kukuwa na kuwa na hali njema. Tunapaswa kukuwa katika
upendo na Mungu. Kama vile kuzaliwa kwa Yesu, Mungu alikuwa karibu kabisa na
ubinadamu, tunapaswa kukuwa katika utakatifu na tunapaswa kukutana na Yesu.
Kukuwa katika utakatifu maana yake kujifunza jinsi ya kuboresha uhusiano wetu
na Mungu kwa sala alisema Mt. Yohane Paulo II.
Tunapaswa
kuwa waangalifu na pia kuwa washiriki katika maisha ya sakramenti katika
Kanisa. Tunapaswa tuadhimishe Ekaristi katika hali inayofaa, kwani “Kila wakati
Kanisa linavyo adhimisha Ekaristi linakumbuka ahadi yake na kujikita katika
yeye “ambaye atakuja”. Katika sala zake linaita ujio wake. “Maranatha!” “njoo
Bwana Yesu” Bwana tunaomba neema zako zije na ulimwengu utapita. (Katakisimu ya
Kanisa katoliki – 1403)
Tamaa
ya kutaka kuwa karibu na Yesu inapaswa kuwa ni tamaa pia ya kutaka kuwa karibu
na ndugu zetu, dada na kaka zetu, kwani hakuna kitu kizuri kwa Mungu kama
kutamani ishara ya huruma ya kweli. Kwa hali yake ya asili huruma na inakuwa
inaonekana katika hali ya matendo Fulani. Hatuitwii tu kuwa karibu na Mungu
bali pia tunaitwa kwakuwa karibu huko kuleta mabadiliko katika maisha yetu na
kwa wote walio karibu nasi,hasa maskini, wagonjwa na wanaoteseka. Tunaomba
neema ya majilio itusaidie kuwa wanyekevu ndani ya mioyo yetu.
Sala:
Bwana, majilio inavyoa anza, mioyo yetu inatamani kupata joto la upendo wako na
akili zetu zinatafuta mwanga wa Neno lako.Tuongezee Imani Mkombozi wetu ujasiri
na kukuwa katika upendo. Nisaidie niweze kufungua masikio yangu na kusikia
sauti yako, na moyo wangu kwa utukufu wako mkuu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment