MASOMO YA MISA, NOVEMBA 25, 2020
JUMATANO,
JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Ufu.
15:1 – 4
Mimi,
Yohane, niliona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, nay a ajabu;
malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu
imetimia. Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na
moto, wa wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa
hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo,
wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa
Mwanakondoo, wakisema.
Ni
makuu, nay a ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za
kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa. Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na
kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa
yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha
kufunuliwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
98:1 – 3, 7 – 9 (K) Ufu. 15:3
(K)
Matendo yako ni makuu, Ee Bwana Mungu Mwenyezi.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Kwa
maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono
wa kuume wake mwenyewe,
Mkono
wake mtakatifu umemtendea wokovu. (K)
Bwana
ameufunua wokovu wake,
Machozi
pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka
rehema zake,
Na
uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. (K)
Bahari
na ivume na vyote viijazavyo,
Ulimwengu
nao wanaokaa ndani yake.
Mito
na ipige makofi,
Milima
na iimbe pamoja kwa furaha. (K)
Mbele
za Bwana;
Kwa
maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu
ulimwengu kwa haki,
Na
mataifa kwa adili. (K)
SHANGILIO
1Thes.
2:13
Aleluya,
aleluya,
Lipokeeni
neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:12-19
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake; Watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya
masinagogi, na kuwatia magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa
ajili ya jina langu. Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu. Basi, kusudieni mioyoni
mwenu, kutofikirifikiri kwanza mtakavyojibu; Kwa sababu mimi nitawapa kinywa na
hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga. Nanyi
mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao
watawafisha baadhi yenu. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.
Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. Nanyi kwa subira yenu
mtaziponya nafsi zenu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment