“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Novemba 25, 2020,
Juma
la 34 la Mwaka wa Kanisa
Ufu
15:1-4;
Zab
97:1-3, 7-9;
Lk
21:12-19
UVUMILIVU
UTAOKOA MAISHA YENU!
Ndugu
zangu karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo.
Kwa
uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu. Haya ni maneno ya injili ya Yesu leo
anapotueleza juu ya ujio wa ujio wa siku za mwisho na vishawishi viwezavyo
kutufanya tupoteze imani yetu.
Anatueleza
kwamba njia ya kufikia mbinguni sio rahisi, yahitaji uvumilivu mkubwa.
Unapotaka kumtumikia Bwana, shetani anakuja pia karibu akiwa na lengo la
kukuzuia ili Bwana asipate mtumishi. Atajitahidi kuleta kila aina ya vishawishi
na mateso.
Enzi
za mitume, mateso yaliyoletwa na shetani ni kutengwa na ndugu zako wa damu kwa
sababu ya mtu kuiacha dini yake ya asili hivyo unatengwa na kuchukiwa na
wajomba, kaka, dada na wazazi na pengine wanakufukuza hata nyumbani. Pia
kulitokea watawala waliowachukia wakristo na kuwatesa wakitaka waikane imani
yao.
Hizi
zote ni njia alizotumia shetani kuiangusha injili. Siku hizi kwa sababu ya
uwepo wa utawala wa sheria na uteteaji wa haki za kibinadamu shetani amegeuza
vishawishi vya kutufanya tusimtumikie Kristo na hivyo tuikose mbingu. Hivi ni
vishawishi kama kuanzishwa kwa kumbi nyingi za starehe au ushabikiaji wa
michezo mbalimbali inayotufanya hata tukose kanisani-mfano kipindi cha kombe la
dunia wengi tunakosa kanisani pengine tukitaka kuangalia mechi.
Pia
kutumia muda mwingi katika simu. Njia zote hizi zaweza kutufanya tushindwe
kumtumikia Mungu.
Kwenye
somo la kwanza tunaambiwa kwamba ni waliopata ushindi ni wale waliopitia katika
dhiki iliyokuu na hawa wanapata nafasi ya kumshangilia Mungu kwa matendo yake
makuu ya kuwakomboa. Sisi tumshukuru Mungu kwani kila siku anatupigania na
kutupatia pumzi, na amani, na kazi na marafiki wazuri wanaotuzunguka. Tuanze
kumtukuza Mungu kwa wimbo kama huu kila kila mara.
Tuache
kumpatia shetani sifa kila kukicha kwa kuwaza au kuongea maneno machafu,
kuangalia picha mbaya au vichekesho vya dhambi. Tujitahidi basi hata kuangalia
filamu za Yesu, Bikira Maria na watakatifu na kusoma Biblia kuliko kuongea
maneno machafu kila siku na kumshushia Mungu utukufu wake. Sisi tumpatie
Mwenyezi Mungu utukufu wake kwani anastahili kama tulivyoadhimisha jumapili ya
Kristo Mfalme.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment