Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

NOVEMBA, 2020, JUMATATU, JUMA LA 34 LA MWAKA

 NOVEMBA, 2020, JUMATATU, JUMA LA 34 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA WAT. CLEMENT I NA KOLUMBANI


SOMO 1: Ufu. 14:1-5

Mimi, Yohane, niliona, na tazama, huyo Mwanakondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini nan ne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakavipiga vinubi vyao; na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wane, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi. Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwanakondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwanakondoo. Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.


Zab. 24:1-6 (K) 6

(K) Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.


INJILI: Lk. 21:1-4

Yesu aliinua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Akasema, Hakika nawaambieni,huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote: Maana hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.

No comments:

Post a Comment