“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Novemba 18, 2020,
Juma
la 33 la Mwaka wa Kanisa
Ufu
4:1-11
Zab
150: 1-6
Lk
19:11-28
KUWA
WAZALISHAJI KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU!
Mfano
wa leo kutoka katika Injili, wakati Mfalme alivyorudi, alihitaji hesabu kutoka
kwa kila mtumishi. Kwa njia hii kila mmoja wetu atatoa hesabu ya jinsi tulivyo
tumia vizuri talanta na vipiji tulivyopewa na Mungu. Kati ya Wayahudi waliokuwa
katika mstari wa Mafarisayo, wao walidhania Mungu kuwa hakimu mkali
aliyewatenda kadiri ya faida waliopata kwa kushika sheria. Hali hii iliwajengea
watu hofu na wakashindwa kukuwa. Na zaidi sana, iliwafungia hata wao wenyewe
kushindwa kufungua mioyo na kukubali hali mpya ya kukutana na Mungu alioleta
Bwana wetu Yesu Kristo. Je, wewe na mimi tukoje? Tumetumiaje, au tunatumiaje vipaji
alivyotupa Mungu? Je, tutakana uaminifu wake kwetu?
Sala:
Baba, nakushukuru kwa kuni amini mimi na kunipa vipaji na nafasi, yote
yaliotoka katika mikono yako. Nisaidie mimi nijifunze kuwa mzalishaji wa kweli
kwa ajili ya ufalme wako. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment