MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 18, 2020
JUMATANO,
JUMA LA 33 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Ufu.
4:1 – 11
Mimi,
Yohane, niliona mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia
kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami
nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Na mara nalikuwa
katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu
ya kile kiti; na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki,
na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya
zumaridi.
Na
viti ishirini na vine vikilizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti
naliona wazee ishirini na wane, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya
vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. Na katika kile kiti cha enzi kunatoka
umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto ziliwaka mbele ya kile kiti cha
enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
Na
mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri;
na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye
uhai wane, wamejaa macho mbele na nyuma. Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa
mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai
wa tatu alikuwa na uso kama uso wa Mwanadamu; na mwenye uhai wan ne alikuwa mfano
wa tai arukaye.
Na
hawa wenye uhai wane, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani
wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema:
Mtakatifu,
Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na
atakayekuja. Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Na
hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima,
na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele, ndipo hao wazee ishirini na
wane huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia
yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kiti cha
enzi, wakisema, Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na
heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya
mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
150 (K) Ufu. 4:8
(K)
Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi.
Aleluya.
Msifuni
Mungu katika patakatifu pake,
Msifuni
katika anga la uweza wake.
Msifuni
kwa matendo yake makuu;
Msifuni
kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. (K)
Msifuni
kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni
kwa kinanda na kinubi;
Msifuni
kwa matari na kucheza;
Msifuni
kwa zeze na filimbi. (K)
Msifuni
kwa matoazi yaliayo;
Msifuni
kwa matoazi yavumayo sana.
Kila
mwenye pumzi na amsifu Bwana.
Aleluya.
(K)
SHANGILIO
Yn.
8:12
Aleluya,
aleluya,
Mimi
ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,
bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
INJILI
Lk.
19:11 – 28
Makutano
waliposikia, Yesu aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na
Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara. Basi
akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme
na kurudi. Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha,
akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. Lakini watu wa mji wake
walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
Ikawa
aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha,
ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. Akaja wa kwanza, akasema,
Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. Akamwambia, Vema,
mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na
mamlaka juu ya miji kumi. Akaja wa pili, akasema, Bwana fungu lako limeleta
mafungu matano faida. Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
Akaja
mwingine akasema, Bwana hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika
leso, Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna
usichopanda. Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako mtumwa mwovu wewe.
Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na
faida yake? Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe
yule mwenye mafungu kumi. Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi, Nawaambia,
Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho
nacho.
Tena,
wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwanchinje mbele yangu.
Na
laipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment